Labels

Tuesday, October 2, 2012

“UTAIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI”. Isaya 58:12


 Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu ,hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele”
 Warumi 10:9 “Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chacko ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu uataokoka”
 Huenda mpendwa msomaji wangu hujaokoka na unataka kuokoka. Sasa kabla hujafanya maamuzi ya kuokoka ngoja kwa kifupi nikueleze nini maana ya kuokoka ili uweze kujua ni maamuzi ya aina gani unayoyafanya.
Kuokoka kwa kifupi maana yake ni kumkaribisha YESU katika maisha yako kwa kumruhusu achukue nafasi ya  utawala katika maisha yako. Unamruhusu atawale kwa kumkiri kwa kinywa chako na kuamini katika moyo wako, ya kwamba hakika yeye ni Bwana na Mungu alimfufua sikuya tatu katika wafu.
Kuokoka siyo kuchanganyikiwa, kupotea, ujinga au kufeli katika maisha. Unapoamua kuokoka unakuwa umempa Mungu nafasi ya;
* Kukujulisha kusudi la yeye kukuleta duniani.
*Kukujulisha mawazo na njia zake za kukufanikisha katika mambo yote.
*Unakuwa umejihakikishia uzima wa milele maadam ukiishi katika mapenzi ya Mungu.
*Mwisho unakuwa umempa Mungu nafasi ya kushughulika na maisha yako, afya yako, usalama wako,Uponyaji nk.
Sasa baada ya haya naamini unaelewa aina ya maamuzi unayotaka kufanya. Kama uko tayari kuokoka sema maneno yafuatayo kwa Imani
Sema “Bwana Yesu,  ninakuja  mbele mbele zako, ninakiri ya kuwa mimi ni mwenye dhambi, naamini kweli ulikufa na kufufuka ili nipate kuokoka, nami nayakabidhi maisha yangu kwako uyatawale na ufanyike Bwana wa maisha yangu.
Baada ya sala hiyo, nikupongeze kwa kuwa umefanya maamuzi bora zaidi maishani mwako. Unatakiwa kufanya yafuatayo;
*Tafuta mtu yeyote unayejua naye ameokoka halafu mjulishe uamuzi wako pia.
*Kama hauna kanisa unalosali, basi nenda kanisa lolote linaloamini wokovu pia kisha waambie juu ya uamuzi wako.
*Jenga mazoea ya kusoma neno la Mungu kila siku na kuomba pia. Kadri unavyohudhuria kanisani utajifunza zaidi juu ya kuukulia wokuvu.
*Mwisho naomba pia nijulishe juu ya uamuzi wako kupitia anuani zangu zilizopo kwenye category ya kuhusu Patrick.
Ubarikiwe sana.    
                         By :Meshack Kitova

No comments: