Rafiki yangu:Ninakuuliza swali muhimu maishani mwako. Furaha yako ya
milele au huzuni yako ya milele inategemea jibu Ia swali hili. Swali ni
hili:Je, umeokolewa?Si swali la jinsi ulivyo mwema, wala si swali la kama u
mshiriki wa kanisa, bali:Je, umeokolewa?
Una uhakika kwamba utaenda mbinguni utakapokufa?
Mungu anasema kwamba, ili uende mbinguni, ni
lazima uzaliwe mara ya pili. Katika Yohana 3:7, Yesu alisema kwa Nikodemo,
“Ni lazima uzaliwe mara ya
pili.”
Katika Biblia Mungu anatupatia njia ya pekee ya
kuzaliwa mara ya pili, yaani kuokolewa.Njia
yake ni rahisi! Unaweza kuokolewa leo. Vipi?
Kwanza, rafiki yangu, ni lazima utambue
kwambawewe u mwenye
dhambi.“Kwa sababu wote wamefanya
dhambi,na kupungukiwa na utukufu wa
Mungu”(Warumi 3:23).
Kwa sababu u mwenye dhambi,umehukumiwa kufa.“Kwa
maana mshahara wa dhambi ni mauti”(Warumi
6:23). Hii ina maana kutengwa na Mungu katika jehanum milele.“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya
kufa hukumu”(Waebrania 9:27).
Lakini Mungu alikupenda mno hata akamtoa Mwanawe pekee, Yesu, ili azichukue dhambi zako na
kufa pahali pako.“Yeye asiyejua
dhambi[Yesu, ambaye hakujua dhambi yo
yote]alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili
sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye”(2
Wakorintho 5:21).
Ilimbidi Yesu amwage damu yake na
kufa.“Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo
damu”(Mambo ya Walawi 17:11).“. . . Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo[msamaha]”(Waebrania 9:22).
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu
sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye
dhambi”(Warumi 5:8).
Ingawa hatuelewi ni jinsi gani, Mungu alisema kuwa
dhambi zangu na dhambi zako ziliwekwa juu ya Yesu naalikufa pahali petu.Yesu akawafidia
yetu[badala yetu].Ni kweli. Mungu hawezi kusema uongo.
Rafiki yangu,“Mungu . . . anawaagiza watu wote wa kila mahali
watubu”(Matendo 17:30). Kutubu huku au toba
hii ni badiliko la nia akilini; kukubaliana na Mungu kuwa mtu ni mwenye dhambi,
na kukubaliana na yale aliyoyafanya Yesu kwa ajili yetu msalabani.
Katika Matendo 16:30-31, mlinzi wa gereza wa
Filipi aliwauliza Paulo na Sila,“Mabwana,
yanipasa nifanye nini nipatekuokoka?Wakamwambia,mwaminiBwana Yesu, nawe
utaokoka . . . .”
Mwamini tu Bwana Yesu ambaye alibeba dhambi zako,
akafa badala yako, akazikwa, na Mungu alimfufua.Ufufuo wake unahakikisha kwa nguvukuwa aaminiye anaweza kudai uzima wa milele anapompokea
Yesu kuwa Mwokozi wake.
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika
watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”(Yohana 1:12).
“Kwa kuwakilaatakayeliitia jina la
Bwanaataokoka”(Warumi 10:13).
Neno“kila”linakujumlisha na wewe.“Ataokoka,” maana
yake si labda, au inawezekana, bali ni kwa uhakika“ataokoka.”
Hakika, unatambua kuwa u mwenye dhambi? Po pote
ulipo sasa hivi, ukitubu, inua moyo wako kwa Mungu katika maombi.
Katika Luka 18:13, mwenye dhambi mmoja
aliomba:“Ee Mungu, uniwie radhimimi mwenye dhambi.”Basi
omba:“Ee Mungu, ninajua kuwa ni mwenye
dhambi. Ninaamini kuwa Yesu alikuwa fidia yangu alipokufa msalabani. Ninaamini
damu yake aliyomwaga, kufa kwake, kuzikwa kwake, na kufufuka kwake kulikuwa kwa
ajili yangu. Sasa ninampokea awe Mwokozi wangu. Asante kwa msamaha wa dhambi
zangu, zawadi ya wokovu na uzima wa milele, kwa sababu ya neema yako ya huruma.
Amina.”
Mwamini Mungu katika Neno lake, na dai wokovu wake
kwa imani. Amini, na utaokoka. Hakuna kanisa, wala jumba, wala matendo mema
yawezayo kukuokoa.Kumbuka, Mungu ndiye
aokoaye. Basi!
Njia rahisi ya wokovu ya Mungu
ni:Wewe u mwenye dhambi na usipomwamini
Yesu ambaye alikufa pahali pako, utakaa milele jehanum. Ukimwamini kuwa Mwokozi
wako ambaye alisulubiwa, akazikwa, akafufuka, utapokea msamaha wa dhambi zako
zote, na utapokea zawadi [karama] ya uzima wa milele kwa imani.
Unasema, “Kweli, haiwezi kuwa rahisi
hivi.”Ndiyo, ni rahisi hivyo! Ndivyo ulivyo
mpango wa Mungu wa wokovu katika Maandiko.Rafiki yangu, mwamini Yesu na kumpokea kuwa Mwokozi wako
leo.
Ikiwa huu mpango wake wa wokovu hauko wazi au
haueleweki kwako, soma kijikaratasi hiki tena na tena, pasipo kukiweka chini,
mpaka umeuelewa ujumbe wake. Nafsi yako ni ya thamani zaidi kuliko vyote vya
ulimwengu.
“Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu
wote, akipata hasara ya nafsi yake?”(Marko
8:36).
Hakikisha kwamba umeokoka. Ukipoteza nafsi yako
utapoteza mbingu na utapoteza vyote. Tafadhali, mruhusu Mungu akuokoe sasa
hivi.
Nguvu ya Mungu itakuokoa, itakulinda, na
kukuwezesha kuishi maisha ya ushindi ya Kikristo.“Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya
wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo;
lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze
kustahimili”(1 Wakorintho 10:13).
Usitegemee hisia zako – jinsi unavyojisikia. Hisia
zinabadilika-badilika. Simama juu ya ahadi za Mungu. Ahadi za Mungu
hazibadiliki. Ukiisha kuokoka, kuna mambo matatu ya kufanya kila siku ili ukue
kiroho:Omba– unazungumza na Mungu.Soma Biblia yako–
Mungu anazungumza nawe.Shuhudia– waambie
watu wengine kwa niaba ya Mungu.
Unapaswa kubatizwa katika utii kwa Bwana Yesu
Kristo kuwa ushuhuda wa hadhara wa wokovu wako, halafu, bila kuchelewa, jiunge
na kanisa ambalo linaamini Biblia.“Basi usiuonee
haya ushuhuda wa Bwana wetu . . . ”(2 Timotheo
1:8).
“Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami
nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni”(Mathayo 10:32).
No comments:
Post a Comment