Kijana mwenzangu
ninakusalimu kwa jina la Bwana. Katika mwezi huu nina neno fupi ambalo nimeona
ni vema nikushirikishe na wewe juu ya ‘UMUHIMU WA KUUTAFAKARI MWISHO WAKO
UKIUHUSIANISHA NA KUSUDI LA MUNGU JUU YAKO’
Tarehe 26/04/2012
nilifanya maombi maaulumu yaliyolenga kuombea vijana ambao bado hawajaoa au
kuolewa, nikimsihi Mungu afungue milango ya wao kuoa au kuolewa, kwa sababu
wengi wao ninaowasiliana nao bado hawajaoa au kuolewa.
Katika kunijibu Mungu
alinipa mistari kadhaa na kunifunulia tafsiri yake, nami nikaandika kwenye
kumbukumbu zangu na mwezi huu nimeona ni vema na wewe nikushirikishe mafunuo
haya maana naamini yatakusaidia;
Fungu la kwanza ni,
Luka 19:41 – 44.
Soma fungu hili lote, mimi
nitanukuu maneno machache tu. “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, akasema,
laiti ungalijua hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani … siku zitakuja adui
zako watakujengea boma … watakuangusha chini wewe na watoto wako … kwa sababu
hukutambua majira ya kujiwa kwako.
Fungu la pili ni,
Isaya 1:2-3
“Sikieni enyi mbingu tega
sikio ee nchi … kwa maana Bwana amenena; nimewalisha watoto na kuwalea
nao wameniasi, ng’ombe amjua Bwana wake, punda ajua kibanda cha
Bwana wake, bali Israel hajui, watu wangu hawafikiri”.
Fungu la tatu (3) ni ,
Kumbukumbu la Torati 39:29.
“Laiti
wangalikuwa na akili hata wakafahamu haya, ili watafakari mwisho wao”.
Katika mafungu haya matatu
ya maandiko Roho mtakatifu alinifunulia yafuatayo;
*Kwanza alisema, usifikiri
hao watu unaowaombea siwajibu. Wengi nilishawajibu, lakini wengine kwa sababu
zao binafsi, wazazi wao, Viongozi wao n.k hawajatii wazo langu juu
yao/mapenzi yangu juu yao. Mimi ni Mungu ninayeangalia kesho/mwisho wa mtu/watu
na lolote ninalofanya nimeliona mwisho wake. Sasa kwa kuwa hawa vijana
wamekataa wazo langu kwa kutofikiria mwisho wao na kusudi langu kupitia wao na
ndoa zao, basi, hakika ndoa zao
zitakuwa na shida na baadhi yao wataniacha
kabisa.
*Pili, Mungu kwa uchungu
sana anataka mbingu na nchi zisikie na zijue kwamba
watoto wake ambao amewalisha na kulea
wamemuasi. Watoto hao wameshindwa kujifunza kupitia ng’ombe na
punda, na tatizo lao ni kutokufikiri. Hii ina maana kutokufikiri kwao
kumepelekea wao washindwe kumjua Mungu. Kinamuuma sana Mungu,
anapoona watu aliowaokoa na kuwafundisha au kuwaonyesha njia wapasayo kuiendea
wanakataa kwenda katika njia yake.
Zaburi 32:8
anasema “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, nitakushauri
jicho langu likikutazama”. Sasa kitu kinachomuumiza ni pale
anapowaonyesha watu njia yake au mapenzi yake kwao kuhusu wake/waume zao
watarajiwa na akina nani halafu wao wanashindwa kutii. Licha ya kuwaonyesha au
kuwajulisha mapenzi yake bado wameasi.
Ndugu kijana
mwenzangu, natamani Mungu alete kitu hiki ndani yako kwa uzito ule ule aliouleta
ndani yangu, ili usije ukakataa wazo la Mungu kwako na ukamkosea hata kuikosa
mbingu kwa sababu tu ya mke au mume.
Sasa fanya yafuatayo ili
kukaa katika mapenzi yake;
(a) Jifunze kutafakari mwisho
wako, ukijua ya kwamba mwisho wako uko mikononi mwa Mungu. Na kwa sababu hiyo
maamuzi yoyote unayoyafanya ni lazima, na si ombi umruhusu Mungu
akuongoze ili uenende katika njia zake.
(b) Haijalishi kwa jinsi ya
mwili huyo mtu ana upugnufu/udhaifu wa aina gani kwa mtazamo wako, maadam una
uhakika ni mtu wa mapenzi ya Mungu uishi naye, basi usijaribu kukataa huyo mtu
kwa sababu Mungu ameona unakokwenda kukoje na huyo aliyemleta ndiye ambaye
mtafika naye mwisho wenu.
(c) Hivyo basi wazo
lolote/kijana/mtu yoyote anapokuja kwako kutaka muoane na ndani
yako unaona hakika ni mtu wa mapenzi ya Mungu, basi kabla
hujakataa kwa sababu zako binafsi, kaa chini utafakari, mhoji Mungu kwa maswali
yanayokutatiza. Unapokwenda mbele za Mungu siku zote yeye ni mwaminifu atakupa
majibu ya msingi na nina kuhakikishia unapotii uongozi wa Mungu kuna baraka za
ajabu sana. Lakini unaposhindwa kutii itakugharimu kuliko
unavyofikiri.
*Mungu anapokuonyesha/anapokupa mke au mme hamleti
kwako kwa lengo la kukukomoa, bali anakua ameangalia kwanza kusudi lake,
changamoto zilizopo mbele yenu na umbali mnaotakiwa kusafiri kwa pamoja kisha
ndio anawaunganisha kwa kukupa mtu (mke au mume) ambaye anajua ukiwa naye hakika
kusudi lake litafikiwa na mtaweza kuzikabili na kuzishinda changamoto zote
zitakazojitokeza.
Hivyo mwenzi yoyote unayempata kama una hakika katoka
kwa Mungu hata kama ana mapungufu gani kwa fikra zako au wazazi au dhehebu
lako mimi nakushauri usimkatae, kwa sababu kwa huyo wewe utaweza kulitumikia
shauri la Bwana.
Aliye na masikio na asikie lile ambalo Roho wa Bwana
asema na vijana
No comments:
Post a Comment