Katika Biblia Yako SomaIsaya 66; Zaburi 67.
Mstari wa Kukariri
‘…wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia,”Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike,kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu,naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”’ (Isa 41:9,10).
Baadaye Zungumzieni Jambo HiliMwambie mwenzako Msalaba unaweza kumaanisha nini kwako kwa kile ambacho Mungu anaweza kukitaka kwako; pengine atataka uende mahali fulani, au atakuamuru kufanya jambo fulani, au atakuamuru kutoa kitu fulani, au atakuamuru kuacha jambo fulani.
Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana TenaKwa kuzingatia kwamba muda unakwenda mbio na siku ya mwisho inakaribia, hebu fanya maombi kwa upya ukimkabidhi Yesu wenye dhambi wawili kutoka kwenye familia yako au miongoni mwa rafiki zako.
Kazi ya Kuandika Ya StashahadaJe, unauhisi mkono wa Mungu ukiwa juu ya maisha yako ukikuchagua kumtumikia Yesu? Andika ukurasa mmoja wenye maelezo ya kile unachofikiri Mungu anakuitia. Je, unafikiri anakuita uwe nani au ufanye nini?
Tafakari Mistari IfuatayoIsa 43:4-7
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha
Ulimwengu
Ombea Falme za Kiarabu.
Wapo
Waislam 2,200,000 katika majimbo 7; Kuna umaskini kwenye utajiri
mkubwa Huduma ya Kikristo imekatazwa; Hakuna
Kanisa nchini humo
Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.
Katika kitabu cha
Mwanzo, Baba Mungu aliyesalitiwa na kuhuzunishwa, anatembea bustanini wakati wa
jua kupunga akiwatafuta rafiki zake, mwanamume na mwanamke; ambao muda mfupi tu
uliopita wamepoteza imani yao, kwa kuamua kumtii Shetani na kusababisha madhara
makubwa kwa ulimwengu. Maneno ya Baba yanaelezea upendo wake, ‘Adamu uko wapi?’
Na kwa swali hilo haielekei kama Mungu alikuwa anataka kujua alikokuwa
amejificha Adamu! Biblia inatuonesha kwamba Mungu alianza kuweka mambo sawa kwa
kutoa ahadi (Mwa 3:9).
Katika kitabu cha
Mwanzo pia kuna habari za Yusufu, mtu aliyetumwa na Mungu kuokoa taifa (Mwa
37-50).
Katika kitabu cha
Kutoka, Mungu anaonesha uwezo wake wa kuokoa taifa kutoka utumwani. Anataka
kuwabariki kwa kuwafanya taifa la kimishenari kwa kulipeleka Neno lake na uzima
wake kwa ulimwengu wote (Kut 3:7-19:6).
Katika Zaburi,
Mungu ameuonesha upendo wake mara kwa mara (Zaburi 67, Zaburi 2, Zab 72:17).
Manabii na manabii
wadogo kama Yona walijazwa na uwezo wa kimbingu, japo kwa vipindi vidogovidogo,
wa kuupenda ulimwengu (Isa 6:1-8; Isa 54:1-5; Hab 2:14)..
Mpango wa Mungu kwa ulimwengu wote
unadhihirishwa na Nabii Isaya anaposema kwamba kuna mambo manne anayokusudia
Mungu kuyafanya; vilevile yapo mambo mawili ambayo Mungu anataka sisi tuyafanye
(Isa 66:18-21).1. Mungu anasema, ‘Ninakaribia Kuja’
Katika Isa 66:18, huu ni ufunuo wa kinabii kuhusu Kuja Mara Ya Pili kwa Kristo. Wakati huo atawakusanya mataifa yote pamoja kutokana na vitendo vyao na hisia zao. Hakuyafanya hayo alipokuja mara ya kwanza. Tutalijadili hilo baadaye na kuona ishara duniani na katika Ufalme zinazoashiria kurudi kwa Yesu.
Maana yake ni kwamba ipo siku ya mwisho. Hizi ni
habari njema kwa kila mwamini, lakini pia ina maana kwamba kuna siku ya mwisho
kwa kila mmoja wetu kuwaleta kwa Yesu jamaa zetu, rafiki zetu, na mataifa.
2. Nitafanya Ishara
Miongoni MwaoIshara katika Isa 66:19 ni Msalaba, na huu unajulikana ulimwengu mzima. Kwa asiyeamini, Msalaba ni tamko la dhahiri la upendo mkuu wa Mungu kwa ulimwengu wote (Yn 3:16) Lakini kwa kila aaminiye, Msalaba una maana kubwa zaidi. Kalvari ilianzia Gethsemane na Yesu katika ubinadamu wake Msalaba ulimaanisha mapambano ya:
Kwenda asikotaka kwenda,
Kufanya asichotaka kukifanya,
Kutoa asichotaka kukitoa.
(Mt 26:39) (Lk 9:23)
Hapakuwa na njia nyingine. Na kwa
furaha iliyokuwa mbele yake, furaha ya kukuona wewe ukiwa salama mbinguni, Yesu
aliuvumilia Msalaba. Sisi nasi yatupasa kuvumilia kwa ajili ya wengine (Ebr
12:2).3. Nitawapeleka Katika Mataifa Baadhi ya Wale Waliopona
Mbali sana; Hispania, Libya, Asia, Ugriki,na baadhi ya visiwa (Isa 66:19). Leo hii watu wa makanisa ya mataifa yaliyoendelea wanafanana sana na watu wa ulimwengu na ambao hawajafikiwa na Injili. Kwa ajili ya hao Yesu ataita watu na kuwatuma mbali sana kama wamishenari.
Je, unapaswa kupona nini?
Unapona mateso ya Msalaba na hitaji lake la kifo na
kufanya mapenzi ya Mungu kwa gharama zote (Lk 9:23).
Unaponaje?
Ni ajabu, unapona tu na kuokoa maisha yako kwa
kukubali kupoteza maisha yako kwa ajili ya Yesu na mapenzi ya Mungu (Lk 9:24).
Sasa tutaangalia na kuona yale
mambo mawili ambayo tunapaswa kuyafanya ikiwa ni mwitikio wetu kwa wito wa Mungu
wa kutumwa. Mambo yenyewe si magumu sana.4. Watautangaza Utukufu Wangu
Je, utukufu wa Mungu ni nini? Ni Mungu aishiye Mwenyewe. Tunatangaza uwepo wake, upendo wake, nguvu zake, uweza wake, huruma zake na neema yake. Tunamtangaza Mwanaye, maisha yake, kifo chake, kufufuka kwake, na kwamba yu hai leo na anaweza kuokoa, kusamehe, kuponya, kuweka huru, na kuwajaza watu na Roho wake. Na ndipo utukufu wake unakuwa dhahiri kwa maisha yaliyobadilishwa (Isa 66:19; Mdo 1:8).
5.Watawaleta Ndugu Zako Wote
Mara zote Injili itafanya kile kilichoahidiwa kwenye Injili, na mwitikio wa watu ni kumfuata Yesu (Isa 66:20; Yn 12:32). Tutawaleta hadi mlima wake mtakatifu-hili likimaanisha ufuasi miguuni pa Yesu, (k.m. Mt 5:1).
Je, waamini wapya watatoka wapi?
Watakuja wamepanda farasi - ikiwa na maana ya mataifa ambayo hayajafikiwa ya Asia ya Kati. Tangu mwanzo farasi wengi walitokea eneo hilo.
Watakuja wamepanda magari - ikiwa na maana ya watu waliorudi nyuma kutoka mataifa ya Magharibi.
Watakuja wamepanda vihongo – ikimaanisha watu kutoka mataifa yanayoendelea.
Watakuja wamepanda ngamia – ikiwa na maana ya watu kutoka mataifa ya Kiarabu kwenye Uislamu.
6. Nitachagua Baadhi Kuwa Makuhani
Hatua ya mwisho ya ufunuo wa Nabii Isaya ipo katika mstari wa 21 (Isa 66:21). Ni unabii ulio sahihi kabisa kuhusu mambo ambayo Mungu anayafanya sasa katika ulimwengu mzima. Anawaita wanaume na wanawake walioamua kumfuata Bwana, kutoka watu wa mataifa yote na tamaduni zote, kuacha yote na kumfuata Yesu. Tunaweza kumwona mwamini mchanga akipambana ili kuwa huru na dhambi, lakini Yesu anaona uwezekano wa mwamini huyu kuwa mtu wa Mungu, na anamchagua kuhudumu (Mk 1:17).
Mordecai Ham ni Mwinjilisti Mmarekani ambaye hakujulikana sana; na katika kuhubiri kwake katika mji mmoja zamani sana, hakujua kwamba kijana mmoja aliyetoa maisha yake kwa Yesu jioni ile baadaye angekuwa mhubiri mkubwa akiwahubiria mamilioni ya watu kote ulimwenguni katika muda mrefu wa huduma yake. Je, wamfahamu kijana huyo? Alikuwa ni Billy Graham ambaye jioni ile Mungu alimchagua kwa makusudi yake matakatifu.
Kwa
Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu
Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili Ya Yesu Kristo
Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili Ya Yesu Kristo
Burkina Faso | ||
Jina la
Watu
|
Lugha
Yao
|
Idadi Yao |
Djan (Dian, Dyan)
|
Dian
|
14,100 |
Seemogo
|
Sambla (Seeku)
|
17,000 |
Senabi (Niangolo)
|
Senoufo, Senar (Nyangola)
|
50,000 |
Syem (Karaboro, Western,
Syer)
|
Karaboro, Western
|
19,500 |
No comments:
Post a Comment