Na
Mt. Meshack Ezekia Kitova
Yoshua 1:8 “kitabu hiki cha Torati kisiondoke kinywani mwako, bali
yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa
na maneno yote yaliyoandikwa humo……..)
Hapa tunaona jinsi Mungu alivyomtisitiza Joshua kwa habari ya kulitafakari neno la Mungu usiku na mchana .
Lengo la waraka huu mfupi kwako mpendwa msomaji ni kukueleza sababu
za msingi kwa nini ni lazima na sio ombi kwamba usome na kulitafakari
Neno la Mungu usiku na mchana.Kabla sijakueleza sababu nikupe tafasiri
ya Neno la Mungu kwa ufupi, neno la Mungu ni jumla ya mawazo ya Mungu
juu ya mwanadamu.
Ndani ya Neno kuna maamuzi (hukumu), sheria, maagizo na njia za Mungu
za kumtoa mwanadamu katika shida aliyonayo, kumfanikisha katika mambo
yote na kumsaidia, kuishi kwa kulishika shauri (kusudi) la Bwana.
Sababu hizo ni ;
(a) uweze kuelewa nini mawazo ya Mungu juu yako .
Katika kitabu cha Yeremia 29:11 Mungu anasema nayajua mawazo
ninayokuwazi si mawazo mabaya ………, sasa ili uweze kuelewa Mungu
anakuwazia nini ni lazima usome kwa kulitafakari neno lake ili upate
anachokueleza kuhusu maisha yako, huduma, kazi, biashara nk.
(b) upate kuifanikisha njia yako.
Yoshua 1:8b. Mungu anasema nitakufundisha na kukuonyesha njia
utakayoiendea ………….( Zaburi 32:8), kumbuka kila mmoja ana njia yake ya
kupita ili kilitumikia shauri la Bwana. Sasa ili uweze kufanikiwa katika
njia yako ni lazima usome na kulitafakari Neno la Mungu maana ni taa ya
miguu yako. Zaburi 119:105.
(c) usimtende Mungu dhambi .
Zaburi 119:11. mwimbaji wa zaburi anasema, moyoni mwangu nimeliweka neno
lako ili nisikutende dhambi. Neno linawekwa moyoni kwa kulitafakari.
Kadri unavyolitafakari kimapana ndivyo linavyokusaidia na kukulinda na
dhambi. Litakuonyesha hila na mitego ya dhambi ya shetani, na litakupa
ushindi kwa kila ushawishi wa adui.
(d)Ili uongezeke kiimani.
warumi 10:17. Ikiwa chanzo cha Imani ni kusikia, na kusikia huja kwa
neno la kristo, maana yake kadri unavyolisoma na kulitafakari Neno la
kristo mara kwa mara, kisha ukajitamkia mwenyewe ili ulisikie hii ina
maana lazima imani yako itaongezeka tu.
(e)Neno limebeba jibu la mahitaji yako.
Zaburi 107:20. kwa kuwa ndani ya neno kuna mawazo na njia (mikakati) ya
kukufanikisha kimaisha, hii ina maana, unapolitafakari licha ya kuelewa
mipango ya Mungu juu yako, pia utaelewa na njia za Mungu za kukuondoa
katika shida uliyo nayo kiroho, kimwili, kindoa , kibiashara nk.
(f)uweze kustawi sana .
Yoshua 1:8b, Biblia inapozungumzia kustawi ina maana ya kutawala na
kumiliki vema, kimapana yale ambayo Mungu ameyaweka chini yako .Mtu
ambaye ndani yake amejaa Neno la Mungu kwa wingi huyo ana uwezo mkubwa
sana wa kutawala na kuongoza watu pia.
(g)Litakupa miaka mingi duniani . Mithali 3:1. Ukilitafakari Neno la
Mungu katika maisha yako.Neno litakupa miaka mingi ya amani (mafanikio)
hapa duniani na kila ulifanyalo litafanikiwa.
(h)uwafundishe wengine kumjua Mungu.
kumbukumbu 6:1-10. Mungu anataka watu wamjue yeye, kwa hiyo pindi
unapotafakari anajifunua kwako, akajifunua kwako anataka uwaambie na
wengine jinsi alivyo na ukuu wake ili wasimsahau yeye
Naamini baada ya kuwa umejua umuhimu wa kusoma na kutafakari Neno la
Mungu usiku na mchana, utaamua kuanza pia kulisoma na kulitafakari usiku
na mchana.
No comments:
Post a Comment