Labels

Sunday, October 7, 2012

Maombi.


Maombi kwa njia ya barua pepe.
KARIBU KATIKA KONA HII AMBAYO WEWE MSOMAJI UNAWEZA KUTUMA MAHITAJI YAKO AMBAYO UNGEPENDA TUWEZE KUOMBA KWA PAMOJA. 
kitabu cha 1Yohana 5:14-15 Biblia inasema “Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15 Na tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba .
Mstari huu ndio  ambao utakuwa mstari wetu wa msingi katika Maombezi yetu kwa njia hii ya Barua pepe. Mzee Yohana anatutia Moyo kwa neno hili kwamba  lolote tumuombalo Mungu haijalishi ni kubwa au dogo maadam tukaomba sawasawa na mapenzi ya Mungu basi tuwe  na  uhakika  anatusikia.
Nimeona Mungu akijibu wengi, akifungua waliofungwa na kuponya wengi katika huduma hii . Nawe amini tu, Bwana atafanya njia kwa ajili yako pia.
 Sasa kama unataka tuweze kuomba pamoja na wewe katika shida/ haja yoyote uliyonayo huenda  ndoa, masomo, familia, wazazi, huduma, kanisa, uongozi, Biashara, kazi, watoto, afya yako,nk. Unaweza ukatuma hitaji lako katika anuani ifuatayo  meshacezekiakitova@gmail.com
Na mara utakapotuma, waombaji wa huduma hii pamoja na wasomaji wa blogu hii (endapo utataka washirikishwe au yawe wazi kwa watu wote), basi tutaendelea kuomba pamoja na wewe. Kitu cha muhimu kumbuka mbele za Mungu hakuna jambo lisilowezekana.
Maana anamwambia Yeremia katika Yeremia 32:27 “Tazama mimi ni BWANA Mungu wa wote wenye mwili;je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?.Sikiliza msomaji mpendwa Hakuna jambo gumu la Kumshinda Bwana.
MUNGU AKUBARIKI, UWE NA IMANI KWAMBA ATAFANYA, MAANA KILA AMWENDEAYE MUNGU LAZIMA  AAMINI KWAMBA YUPO NA KWAMBA HUWAPA THAWABU WAMTAFUTAO

No comments: