Rafiki yangu:Ninakuuliza
swali muhimu maishani mwako. Furaha yako ya milele au huzuni yako ya milele inategemea
jibu Ia swali hili. Swali ni hili:Je, umeokolewa?Si swali la
jinsi ulivyo mwema, wala si swali la kama u mshiriki wa kanisa, bali:Je, umeokolewa?
Una uhakika kwamba utaenda mbinguni utakapokufa?
Mungu anasema kwamba, ili uende
mbinguni, ni lazima uzaliwe mara ya pili. Katika Yohana 3:7, Yesu alisema kwa Nikodemo,
“Ni
lazima uzaliwe mara ya pili.”
Katika Biblia Mungu anatupatia njia ya
pekee ya kuzaliwa mara ya pili, yaani kuokolewa.Njia yake ni
rahisi! Unaweza kuokolewa leo. Vipi?
Kwanza, rafiki yangu, ni lazima
utambue kwambawewe u mwenye dhambi.“Kwa sababu wote
wamefanya dhambi,na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”(Warumi
3:23).
Kwa sababu u mwenye dhambi,umehukumiwa
kufa.“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti”(Warumi 6:23).
Hii ina maana kutengwa na Mungu katika jehanum milele.“Na kama vile
watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu”(Waebrania
9:27).
Lakini Mungu alikupenda mno hata
akamtoa Mwanawe pekee, Yesu, ili azichukue dhambi zako na kufa
pahali pako.“Yeye asiyejua dhambi[Yesu, ambaye hakujua dhambi yo yote]alimfanya kuwa
dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye”(2 Wakorintho
5:21).
Ilimbidi Yesu amwage damu yake na
kufa.“Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu”(Mambo ya
Walawi 17:11).“. . . Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo[msamaha]”(Waebrania
9:22).
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye
mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali
wenye dhambi”(Warumi 5:8).
Ingawa hatuelewi ni jinsi gani, Mungu
alisema kuwa dhambi zangu na dhambi zako ziliwekwa juu ya Yesu naalikufa pahali
petu.Yesu akawafidia yetu[badala yetu].Ni kweli. Mungu
hawezi kusema uongo.
Rafiki yangu,“Mungu
. . . anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu”(Matendo
17:30). Kutubu huku au toba hii ni badiliko la nia akilini; kukubaliana na
Mungu kuwa mtu ni mwenye dhambi, na kukubaliana na yale aliyoyafanya Yesu kwa
ajili yetu msalabani.
Katika Matendo 16:30-31, mlinzi
wa gereza wa Filipi aliwauliza Paulo na Sila,“Mabwana,
yanipasa nifanye nini nipatekuokoka?Wakamwambia,mwaminiBwana
Yesu, nawe utaokoka . . . .”
Mwamini tu Bwana Yesu ambaye alibeba
dhambi zako, akafa badala yako, akazikwa, na Mungu alimfufua.Ufufuo
wake unahakikisha kwa nguvukuwa aaminiye anaweza kudai uzima wa milele
anapompokea Yesu kuwa Mwokozi wake.
“Bali wote waliompokea aliwapa
uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”(Yohana
1:12).
“Kwa kuwakilaatakayeliitia
jina la Bwanaataokoka”(Warumi 10:13).
Neno“kila”linakujumlisha na wewe.“Ataokoka,”
maana yake si labda, au inawezekana, bali ni kwa uhakika“ataokoka.”
Hakika, unatambua kuwa u mwenye dhambi?
Po pote ulipo sasa hivi, ukitubu, inua moyo wako kwa Mungu katika maombi.
Katika Luka 18:13, mwenye dhambi
mmoja aliomba:“Ee Mungu, uniwie radhimimi mwenye
dhambi.”Basi omba:“Ee Mungu, ninajua kuwa ni mwenye
dhambi. Ninaamini kuwa Yesu alikuwa fidia yangu alipokufa msalabani. Ninaamini
damu yake aliyomwaga, kufa kwake, kuzikwa kwake, na kufufuka kwake kulikuwa kwa
ajili yangu. Sasa ninampokea awe Mwokozi wangu. Asante kwa msamaha wa dhambi
zangu, zawadi ya wokovu na uzima wa milele, kwa sababu ya neema yako ya huruma.
Amina.”
Mwamini Mungu katika Neno lake, na dai
wokovu wake kwa imani. Amini, na utaokoka. Hakuna kanisa, wala jumba, wala
matendo mema yawezayo kukuokoa.Kumbuka, Mungu ndiye aokoaye. Basi!
Njia rahisi ya wokovu ya Mungu ni:Wewe u mwenye
dhambi na usipomwamini Yesu ambaye alikufa pahali pako, utakaa milele jehanum.
Ukimwamini kuwa Mwokozi wako ambaye alisulubiwa, akazikwa, akafufuka, utapokea
msamaha wa dhambi zako zote, na utapokea zawadi [karama] ya uzima wa milele kwa
imani.
Unasema, “Kweli, haiwezi kuwa rahisi
hivi.”Ndiyo, ni rahisi hivyo! Ndivyo ulivyo mpango wa Mungu wa wokovu
katika Maandiko.Rafiki yangu, mwamini Yesu na kumpokea kuwa Mwokozi
wako leo.
Ikiwa huu mpango wake wa wokovu hauko
wazi au haueleweki kwako, soma kijikaratasi hiki tena na tena, pasipo kukiweka
chini, mpaka umeuelewa ujumbe wake. Nafsi yako ni ya thamani zaidi kuliko vyote
vya ulimwengu.
“Kwa kuwa itamfaidia mtu nini
kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?”(Marko 8:36).
Hakikisha kwamba umeokoka. Ukipoteza
nafsi yako utapoteza mbingu na utapoteza vyote. Tafadhali, mruhusu Mungu
akuokoe sasa hivi.
Nguvu ya Mungu itakuokoa,
itakulinda, na kukuwezesha kuishi maisha ya ushindi ya Kikristo.“Jaribu
halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni
mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile
jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”(1
Wakorintho 10:13).
Usitegemee hisia zako – jinsi
unavyojisikia. Hisia zinabadilika-badilika. Simama juu ya ahadi za Mungu. Ahadi
za Mungu hazibadiliki. Ukiisha kuokoka, kuna mambo matatu ya kufanya kila siku
ili ukue kiroho:Omba– unazungumza na Mungu.Soma Biblia yako– Mungu
anazungumza nawe.Shuhudia– waambie watu wengine kwa niaba ya Mungu.
Unapaswa kubatizwa katika utii kwa
Bwana Yesu Kristo kuwa ushuhuda wa hadhara wa wokovu wako, halafu, bila
kuchelewa, jiunge na kanisa ambalo linaamini Biblia.“Basi
usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu . . . ”(2 Timotheo 1:8).
“Basi, kila mtu atakayenikiri mbele
ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni”(Mathayo
10:32).
No comments:
Post a Comment