Labels

Tuesday, October 2, 2012

KANUNI ZA UONGOZIWA KIROHO


Mojawapo ya mahitaji makubwa kabisa ya Kanisa la leo ni hitaji la uongozi wa kiroho.
Unongozi unaoelewa na kufuata kanuni za utumishi na uanafunzi.
Tunaishi katika wakati ambao watu wa Mungu wanataaabika na ulimwengu kuangamia kwa
sababu hakuna wachungaji wa kiroho. Badala ya kuwaongoza wale ambao Mungu
amewaweka katika uangalizi wao wa kiroho, viongozi wengi wanajipatia mali, cheo na
madaraka katika migongo ya wale wanaopaswa kuwatumikia. Uongozi kama unavyoelezwa
na maandiko, unahitaji tena kurudishwa katika Kanisa kwa sababu ulikuwa umeshaharibiwa
sana na viongozi wanaotafuta kujineemesha na umevurugwa na utumiaji wa njia za uongozi
zilizo tofauti na maandiko yasemavyo. Damazio anagusia kwamba njia hizi za kidunia za
uongozi zinatumika licha ya ukweli kwamba wana-saikologia wana-endelea kupata matatizo
mengi kwa Programu zao za mafunzo ambazo kila wakati wameendelea kuzitafutia
masahihisho ili kuweza kupata njia iliyo bora zaidi. Anaendelea kusema kuwa "Ni pigo
kubwa, wakati Kanisa (Kwa sababu ya kutokuwepo kwa uongozi wa Kiroho) linapochukua
njia zisizo za ki-biblia kwa ajili ya kuwafundishia viongozi wake kutokana na hizi programu
za wanasaikologia zinazobadilika kila siku na za wanasayansi wa kijamii badala ya neno la
mungu.1 Wakati Kanisa litakapotumia njia zisizo za kimaandiko, litakuja kukuta kuwa
viongozi wake wanashindwa kukutana na mahitaji ya kiroho ya Mwili wa Kristo. Kutimiza
malengo ya huduma za kibiblia, viongozi wanahitaji zaidi ya shahada za darasani, majina
makubwa makubwa, na uwezo mkubwa ki-akili. Kukutana na mahitaji ya kiroho ya Kanisa,
viongozi lazima waishi maisha ya utumishi, wawe na tabia ya Kimungu, wamsikilize Mungu
na wawe na upako wa Roho Mtakatifu. Kwa kifupi ni lazima wawe wafuasi wa Yesu Kristo.
Viongozi wanaoji-neemeshaNjia zisiso za Ki-maa-ndiko za Uongozi Zaidi ya shahada, majina
makubwa na usomi mwingi Mafunzo ya Uongozi ni lazima, si kwa sababu tu nadharia ya
uongozi imeharibiwa, bali pia kwa sababu Kanisa litatawanyika na kuangamia bila mafunzo
hayo. Katika Mathayo 9:36-37, Yesu alifananisha kizazi cha binadamu na kondoo. Hili
halikufanyika kuonyesha dharau, bali kuonyesha ukweli mmoja mkubwa. Kama vile ambavyo
kondoo Uli-nganisho kati ya binadamu na kondoo huko Ghana wanahitaji mchungaji,
binadamu pia wanahitaji viongozi. Katika miaka yetu minne huko Ghana kama wamisionari
ulinganisho huu ulileta maana.Mara nyingi tuliwaona kondoo wakizagaa bila waangalizi wa
mchungaji. Wali - "kula" katika majalala ya takataka, karibu na kijiji tulichokuwa tunaishi
wakijishibisha na vinyesi. Wengine waligongwa na magari. Hapakuwepo mtu wa
kuwaongoza kwenye majani mabichi au kuwalinda kutoka kwenye hatari. Watu, katika
namna nyingi wanafanana na kondoo. Wakiachwa wenyewe watazurura huku na huko
wakijishibisha na "takataka" za dunia hii, wakihatarisha roho zao yawezekana kuendelea
milele. Kwa sababu hiyo Kristo aliwaonea huruma. Ulimwengu unahitaji viongozi wa kiroho
watakaosimama kijasiri katika kizazi kilichopotoka (Wafilipi 2:5) wakielekeza, na kuongoza
kwa mfano na kutangaza kikamulifu ushauri wa Mungu.
Yesu aliteua uongozi wa Kanisa (Waefeso 4:11) na aliwafundisha viongozi wake wa mwanzo
yeye Mwenyewe. Inasemekana nkwa usahihi kabisa kwamba Kanisa halijapata tena msukomo
mkubwa wa kiroho kutoka kwa viongozi wake zaidi ya ule wa mitume wa kwanza.2 Ili
kukamilisha kazi yake Kanisa linahitaji kufuata mfano uliowekwa na Bwana wake. Kwa hiyo,
viongozi wa sasa, lazima wamruhusu Bwana kuwatayarisha kwa huduma katika Kanisa na
7
jamii. Ni muhimu kabisa kuelewa na kujiandaa kwa wajibu mkubwa uliopo juu ya viongozi
wa kiroho.
Katika kitabu hiki tutajaribu basi kutimiza yafuatayo:
1. Kuonyesha umuhimu wa uongozi wa kiroho na kuonyesha mambo ya lazima na sifa
zinazohitajika kwa viongozi wa kiroho.
2. Kuonyesha baadhi ya kazi muhimu za viongozi wa kiroho, na pia baadhi ya namna
mbalimbali muhimu za uongozi.
3. Kuonyesha gharama iliyopo ambayo kwayo viongozi wa kiroho `wanajaribiwa'
/wanatahiniwa.
4. Kuonyesha hatari au ugumu katika uongozi wa kiroho na kupendekeza njia
mbalimbali za kushinda majaribu katika huduma (mitego).
-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.-.

No comments: