Labels

Sunday, October 7, 2012

KUSUDI LA MUNGU … SASA!


Nilikuwa nikitazama filamu kuhusu Albert Einstein. Ikianza kulikuwa na kifungu kilichosema kitu kama, “Kila wakati baada ya mda mrefu sana, mwanadamu huja na kuona ulimwengu kupitia macho tofauti na kubadilisha ulimwengu anamoishi.” Tunataka kuweka changamoto hiyo mbele yako. Kuwa aina ya mtu yule ambaye Anaona ulimwengu, sio kupitia kwa macho ya kawaida, bali kupitia macho ya Kiroho. Pata changa moto ya kuwa mmoja wa watu wale ambao Waebrania 11 inawazungumzia kuwahusu. Ona maono ya Mungu ya makao ya Mungu na roho na utukufu unaoongezeka daima. Ona picha katika macho ya akili yako, kama inavyosema kwamba waumini katika kitabu cha Waebrania 11 walivyo ona. Waliona Mji ambao Mjenzi na Mtengenazaji alikuwa Mungu, na kwa hivyo hawakurithika na kitu kingine chochote. Hawakuwa tayari kurudi mji wa zamani. Waliona Mpango wa Mbinguni kwa mbali, na hata kama hawangeweza kuishika na mikono yao, hata kama hawangeweza kuishi ndani ya Mji huo ambao Mungu aliwapangia, hawakuwa tayari kurudi nyuma. “Kwa hivyo, Mungu hakuona haya kuitwa Mungu wao na hao watu Wake.”
Chango moto hiyo moja iko mbele yako wewe na mimi. Angalia dunia unayoishi, ulimwengu unamoishi, na haswa “kanisa” ulilo ndani yake na utamani Nyumba ya Baba ikuchukue. Na tamaa Yake ikuchukue kwa njia ambayo utakuwa tayari kuhatarisha kila kitu katika maisha yako ndiposa uone hiyo ikikamilika katika mazingira yako. Unaweza kuhatarisha maisha yako. Unaweza kuhatarisha familia yako (Zaburi 69:8-9). Unaweza kuhatarisha kazi yako. Unaweza kuhatarisha kila kitu kwa ajili ya Mungu na madhumuni Yake. Hapo ndipo tunapotoka. Kuzungumza Kibiblia hiyo kwa kweli ndiyo aina ya pekee ya Ukristo uliopo. Hilo si fikra au wazo linalojulikana sana. lakini katika Warumi 4 inasema , “Wale waliyo na imani ya Ibrahimu ni wana wa Ibrahimu.”
Kwa hivyo, haijalishi hali yoyote ile au kanisa ulioko, na mahali unaweza kuwa ( nchi yoyote au makao ambayo unayo na uitayo nyumbani kwa sasa), unastahili kuwa mwangalifu sana ili usikubali chochote ambacho Mungu hakubali. Usikubali kwa ajili ya uvivu, kutokujua Neno la Mungu, au ukosefu wa maono au dhambi katika maisha yako ya kibinafsi ambayo imekuziba au kukujeruhi hadi unahisi hautoshi. Usiruhusu wengine ambao wametoshelezwa na Lao wakusaliti au kukukejeli ili uwe fugufugu.
Pengine umeuziwa ukweli kwamba wewe ni “walai” tu na hauna chochote cha kutoa. Pengine unadhania maoni yako hayana umuhimu kwa sababu kuna watu wengi huko nje wenye hekima na waliosoma… “Wewe unajua Ni nini?” Ninataka kukuhimiza kwamba haijalishi wewe ni nani, una kitu cha kutoa. Ikiwa kwa kweli umeitwa kwa jina la Bwana na umemwuliza achukue usukani wa maisha yako, una kitu cha kutoa. Ikiwa umemwuliza akuoshe dhambi zako, una kitu cha kutoa. Haja Yake ni kwamba kuanzia mdogo hadi mkubwa na kila mtu amjue Yeye, aishi katika baraza Lake na ashiriki na Yeye, na Utatu, kila siku.

Mara moja baada ya muda mrefu sana, mtu huja au watu huja ambao wako tayari kushuku ulimwengu wanamoishi na kufanya utofauti katika ulimwengu ulio karibu nao. Waebrania 11 inahusu hiyo. Hiyo ndiyo Mungu ameitia kila mmoja wetu awe ikiwa tuna ujasiri na tuko tayari na tunaushirika na kichwa. Tukikaa ndani Yake, kutakuwa na matunda ya kuonyeshana. Unaweza kuwa mtu ambaye analeta utofauti katika ulimwengu ulimokuwa.
Ninatumaini tumeweka wazi kuto kuelewa moja ambayo imengia katika jamii ya Wakristo. Hiyo ni kwamba kuwa Mkristo ndio mwisho wa hadithi. Na kisha “kuhudhuria kanisa unalolipendelea Jumapili” ni udumishaji hadi Yesu arudi tena na wewe uende kwa nyumba ya kifahari juu ya mlima. Ninataka kuliondoa wazo hilo kabisa kwa sababu hilo si wazo la Mungu. Mungu anaita wazo hilo dini la uongo na Laokia, ambalo linatatiza tumbo Lake.
“Kusudi la Mungu ni kwamba sasa, kupitia kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulishwe viongozi na wenye mamlaka katika ufalme wa mbinguni….” Waefeso 3:10
Hili ndilo kusudi la Mungu SASA HIVI. Mapenzi Yake ni kufanya hekima Yake iliyo ya namna nyingi ijulikane kupitia Kanisa. Sio kupitia watu ambao wameokoka, na wala sio kupitia jamii ya watu wasiyo weza kuzaa ambao wanasikiliza mahubiri siku maalum ya wiki wakiwa wamevaa suti na tai… lakini kupitia kitambaa cha maisha, kupitia jamii ya waumini ambao “wameunganishwa na kushonwa pamoja na kila kano ya kushikilia,” na watu ambao vipawa vyao vimeunganishwa sana, hao “wanashirikiana.” Kuunganishwa, kwa “moyo mmoja, akili moja, kukubaliana pamoja, na kusudi moja.” Pigania maono hayo kwa Matendo ya waumini kutochukua mali, kwa kuunganishwa pamoja—kwa “kujitolea kwa mafunzo ya mitume, kumega mkate, kushirikiana, maombi,” na “kila siku hadharani na kutoka nyumba hadi nyumba.” Fikiria Watu wa Mungu kama ushirika—uliounganishwa, ulio na kitambaa cha maisha cha pamoja ambacho milango ya kuzimu haiwezi kuishinda. Dini ambalo msingi wake ni “mahudhurio” ni sawa kwa Waindi na Waislaamu, lakini sio ile Yesu aliyonzisha na kupaka mafuta.
Kusudi Lake ni “sasa, kupitia Eklesia,” kupitia Ushirika ambao ni wa kweli na wala sio umati wa watu ambao wanahudhuria kitu, bali maisha ambayo yameunganishwa—“kuungamiana dhambi,” kubebeana mizigo” na “kupendana.” Hiyo ndio aina ya maisha ambayo wanadamu wanaweza kuona. Hayo ndiyo aina ya maisha ambayo Yesu alizungumzia kuhusu wakati aliposema “kwa upendo wetu sisi kwa sisi” kuwa “watu wote watajua” imetoka mbinguni (Yohana 13). Alisema kwamba hiyo inaweza “kuaibisha ufalme na mamlaka.” Kusudi la Mungu ni sasa “kupitia Kanisa” ili kuleta aibu hadharani kwa shetani na falme na mamlaka yote. Na kusudi Lake, kulingana na maandiko, ni “SASA” kupitia kanisa ili kuwafanya Adui wake wawe chini ya miguu yake—sio tu kuja Kwake kwa pili na Ufalme mkuu wa Milele, kazi ya Mungu iliyokamilika, bali SASA.
                   Na kwa hakika, hatuzungumzii juu ya jamii kamili. Hatuzungumzii kuhusu sera za jamii, wala sio jambo la baada ya milenia, sio masomo ya utawala. Sio kunyumbua misuli, bali kando na hayo… Tunazungumza kuhusu Watu wakionyesha Maisha ya pamoja kwa njia moja na vile Yesu alionyesha maisha Yake, kama Mfalme wa wafalme wote. Alizaliwa mtoto wa haramu horini, akipanda punda aliye azimwa, na hakuwa na mali yoyote Yake—hakuwa na nguvu, hakuwa na elimu, hakuwa na jukwaa la kisiasa, hakuwa na “urembo au ukuu ambao mtu yeyote angevutiwa.” Tunazungumzia kuhusu kuwa mpenda watu aliyetoka mashinani ambaye angeweza kuona mioyo ya watu na kuwaleta msalabani. Tunazungumza kuhusu kuonyesha watu kashfa ya kuwepo Kwake na maisha Yake, na kuwaita wawe wavuvi wa watu. Wawe sehemu ya Nyumba Yake, “makao” Yake. Wawe mawe yaliyohai. “Ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa.” Huo ndio moyo wa Mungu.

                    Pokea Yesu wa Nazareti, na Ufalme “usio wa ulimwengu huu”, sio kama mshinda Roma au nchi yoyote tunamoishi, au mfumo wa “kanisa.” Mpokee kama Mfalme Seremala aliyependa, na kusemehe, na kutoa maisha Yake…. na yule aliyekuwa tayari kupindua meza za hekalu na kutoa fimbo kama ingehitajika kwa upendo wa Baba Yake na kwa ajili ya Nyumba ya Baba Yake.
Yesu alikuwa tayari kushuku ulimwengu alimokuwa na kwa hivyo kuibadilisha, na ametuita tuwe watu wa aina hiyo. Hii si upitishaji wa habari. Huu ni mwito wa utakatifu na utakaso wa madhumuni ya Mungu, na mwito wa kuinua maono Yake katika mioyo yenu na katika maisha yenu. Piga magoti na uombe. Huu ni mwito, si wa kubadilisha ulimwengu unao onekana tu, bali pia kubadilisha ulimwengu usionekana. “Kusudi Lake ni sasa kupitia Kanisa ili hekima Yake ijulikane, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi, kwa falme na utawala” na kwa watu wote….
Kwa hivyo, hebu kaa linalochoma lisafishe midomo na moyo wako, mwangalie Mungu, na umlilie “Niko hapa, nitume!”

No comments: