Swali: "Je inamaanisha nini kuwa Mungu ni upendo?"
Jibu:
Hebu tuweze kuangalia vile Bibilia inaelezea upendo, na kisha baadaye
tutaangalia namna chache vile Mungu ni sehemu kuu ya upendo. “Upendo huvumilia,
hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabiri; haujivuni; haukosi kuwa na
adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii
udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini
yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote” (1Wakorintho
13:4-8a).Hii ndilo elezo la juu sana la Mungu kuhusu upendo, na kwa sababu Mungu
ni upendo (1Yohana 4:8) hivi ndivyo ilivyo.
Upendo (Mungu)
hajilazimishi/haujilazimishi kwa mtu yeyote. Wale wanaokuja kwake wanafanya
hivyo kwa kuitikia upendo wake. Upendo (Mungu) huonyesha upole kwa watu wote.
Upendo (Yesu) alizunguka kote akifanya mazuri kwa watu wote bila upendeleo.
Upendo (Yesu) hakutamani kitu cha wengine walikuwa nacho, aliishi maisha ya
unyenyekevu bila kunung’unika. Upendo (Yesu) hakujivunia vile alivyo kuwa
kimimwili, ingawa aliweza kumshinda nguvu kila mtu aliyekutana naye. Upendo
(Mungu) haulazimishi unyenyekevu. Mungu hakulazimisha Mwnawe kunyenyekea, lakini
kwa mubadala Yesu kwa pendo lake alimtii Babaye wa mbunguni. “Lakini ulimwengu
ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo.
Ondokeni, twendeni zetu” (Yohana Mtakatifu 14:31). Upendo (Yesu) alitwaza/na
huwaza yaliyo mazuri kwa matakwa ya wengine.
Tibitisho kuu la upendo wa
Mungu limeelezwa kwetu sisi katika Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Warumi 5:8 yakiri ujumbe sawa na wa
Yohana: “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa
Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” Tunaweza kuona
kutoka aya hizi kuwa nia kuu ya Mungu ni tuwe pamoja naye katika mji wake wa
milele, mbinguni. Ameifanya njia rahisi kwa kulipa gharama ya dhambi zetu.
Anatupenda kwa sababu alichagua kwa kutekeleza kifungu cha nia yake. Upendo
husemehe. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata
atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” (1Yohana
1:9).
Je inamaanisha nini Mungu ni upendo? Upendo ni sehemu kuu ya Mungu.
Upendo ni sehemu kuu ya tabia ya Mungu, na utu wake. Upendo wa Mungu kwa
vyovyote vile haugongani/hitilafiana na utukufu wake, utakatifu na haki yake
hata gadhabu yake. Sehemu zote za Mungu kwa pamoja zimekamilika. Chochote Mungu
anatenda hupendeza, haki kwa sababu kila afanyacho hukifanya kwa haki na usawa.
Mungu ni mfano mtakatifu wa upendo wa kweli. Cha kushangaza, Mungu amewapa uwezo
wa kupenda vile anavyo penda, kupitia nguvu za Roho Mtakatifu wale wote
watakaomkubali Mwanawe kama mwokozi wa maisha yao. (Yohana 1:12; 1Yohana 3:1,
23-24).
No comments:
Post a Comment