Labels

Thursday, November 22, 2012

JE! MUNGU NA YESU NI MMOJA?


Makanisa ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo si kama kuwa ni Mwana wa Mungu tu, bali hakika ni Mungu khasa.  Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni mmoja.  Watatu katika mmoja, na mmoja katika watatu.  Wote ni wa milele, wote ni sawa.  Yesu ni Mungu, na Mungu ni Yesu. Hiyo ni imani ya Kikristo, ambayo inaaminiwa na karibu Wakristo wote.  Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili?
Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika:
Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
1 Wakorintho 15.15
Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja hapa anasema: "Tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo." Ikiwa Mungu kamfufua Kristo, hawawezi kuwa wote wawili hao ni mtu  mmoja. Mmoja alikuwa ni mtenda, mfufuaji, na wa pili alikuwa ni mtendwa, mfufuliwa. Kama Kristo ni Mungu mwenye uwezo wa kufufua basi maelekeo ni kusema: "Kristo kajifufua", sio kafufuliwa. Mwenye kufufuliwa ni mfu asiyejiweza kitu.
Katika kitabu cha Matendo ya Mitume inasimuliwa kuwa Mt Stefano alisema aliyoyaona yaliyo mbinguni. Alisema:
Tazama!  naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
      Matendo 7.56
Mwana wa Adamu ndiye Yesu, na kwa jina hilo ndio mwenyewe akipenda kujiita, sio Mwana wa Mungu. Hapo basi huko mbinguni Stefano anasema anamwona Yesu kakaa mkono wa kulia wa Mungu. Mwenye kukaa mkono wa kulia wa fulani hawezi kuwa ndiye yule yule fulani. Hayo ni maelezo ya mbinguni.  Ni wazi basi kwa ushahidi wa Biblia kuwa Yesu hakuwa Mungu mbinguni kama alivyokuwa si Mungu duniani.
Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake.  Huko faraghani aliomba hivi:
Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.  Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
  Luka 22.42-43
Hapa tunaona mambo matatu muhimu:
  1. Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu. Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.
  2. Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: "uniondolee kikombe hiki" cha mauti.  Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake  Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.
  3. Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu."
Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:
Baba ni mkuu kuliko mimi.
Yohana 14.28
Na mwishoni naye yupo mslabani:
Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani?  yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
Mathayo 27.46
Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema: "Mungu wangu naye ni Mungu wenu"?  Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake.  La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo.  Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu.  Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu. 

Tuesday, November 13, 2012

FAHAMU NINI MAANA KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA

 Mt. Meshack Ezekia Kitova    phone;0757672626

 Nini maana ya kusifu na kuabudu


KUSIFU NA KUABUDU ni maneno tofauti na yana maana tofauti
1. kusifu

MAANA --- nikuelezea wasifu au wajihi za kitu au mtu. Sasa tunaposema tunamsifu Mungu inamaanisha ni KWA KUMUINUA JUU, KUSHUKURU KUMPAZIA SAUTI,KUFANYIA SWANGWE, KUJISHUSHA CHINI YAKE KWA UNYEYEKEVU,nk Zaburi 100:4

Neno hili kusifu kwa kiebrania lilikuwa na maana ya;
Tehila, yaani kutamka neno kwa kuongeza vionjo na mbwembwe zaidi. Mfano neno haleluya unalitamka (Ha, ha leluya huuu eee) Tehila ni kuwa kama kichaa unaposifu au kuabudu kwa utukufu wa Bwana. (Nilidhani labda hapa ndipo waswahili walipopata neno taahila).

Yadaa yaani kujiachia kwa Mungu (you just surrender yourself to the Lord).
Barak yaani kusaluti mbele za Bwana. Ni kuonyesha kwamba ni yeye peke yake anayestahili heshima na utukufu. Huwezi kumpigia saluti mtu usiyemwona, hivyo ni kwa njia ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli ndipo tunapomwona kama alivyo na utukufu wake

2. Kuabudu
Neno la Kiebrania shachah lina maana ya kuabudu, kusujudia, kuinama kwa kuonesha unyenyekevu, kuonesha heshima kubwa au kuanguka kifudifudi. Neno la Agano la Kale proskuneo halikadhalika lina maana ya kubusu mkono, au kupiga magoti na kugusa ardhi kwa paji la uso kwa unyenyekevu mkuu. Maneno mengine mawili ya kuabudu yana maana ya kutumika, kufanya ibada Takatifu na kumtolea Mungu Sadaka.

Waache Watu Wangu Waondoke, Ili Wapate Kunitumikia, Dai hili Mungu alilolirudia mara kwa mara lilipelekea Farao kuwaruhusu watu wa Mungu kutoka Misri. Tangu wakati huo, Mungu, Mungu mwenye wivu, amekuwa akipambana na watu wake akiwazuilia kuabudu miungu mingine na sanamu, na badala yake wamwabudu Mungu aliye hai na wa kweli. Kutoka 7:16
Ibada ni kumtukuza Mungu na kumfurahia daima. Mungu anawatafuta watu wa kumwabudu, na kufanya ibada ndiyo wito wetu wa kwanza (Yn4:23 Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. Msitari wa 24 unasema Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.). Ibada ya kweli ni pale tunapomruhusu Roho Mtakatifu atuongoze kutoka katika roho zetu au mioyo yetu kuabudu katika roho na katika kweli na sio tumaini letu ktk miiliau akili zetu Flp 3:3.

Ibada ni tendo la thamani kubwa, ni la kipekee na linamhusu Mungu (utatu mtakatifu) ambao peke yao wanastahili. Lucifer, aliyekuwa mhusika mkuu wa ibada huko mbinguni, alitaka ibada hiyo iwe kwa ajili yake, maana yake aabudiwe yeye badala ya Mungu; na hilo ndilo lililopelekea kuanguka kwake (Isaya 14 na Ezekieli 28). Hata wakati fulani alitaka Yesu amsujudie ili eti ampe falme zote za dunia lakini Bwana alikataa Mt4:8-10.

Kwa hiyo kuabudu ni ibada na tunaposema ibada sio zile taratibu za kibinadamu tulizojipangia katika ibada zetu za siku za leo, ibada za leo tumeweka mambo mengi sana na yanatumia muda mwingi sana kuliko ile maana hasa ambayo mungu aliikusudia katika agano la kale utana ibada zilikuwa zinafaywa kwa mambo makuu 2 neno la Mungu, na Kuabudu.

Kuabudu ni sehemu ya maisha wanadamu tumeumbiwa kuabudu, watuwezi kuishi bila kuabudu hapa haijalishi unaabudu nini!!! Unaweza kuwa unaabudu Mungu wa kweli au miungu kama ambavyo ukisoma bilia utaona kuna miungu mingi inatajwa mfano Baali, Dagon ink na hata leo iko miungu mingi ambayo wanadamu wanaiabudu lakini wa kuabudiwa ni mmoja tu. Na katika biblia tunaona kuaudu kwa mara ya kwanza kulikofanywa na Ibrahimu kutoka katika kitabu cha mwanzo 12: 8 Psalms 34:1 inaonyesha tunatakiwa kumwabudu Mungu kila wakati.

Kwanini tuabudu
kuabudu ni agizo kutoka kwa Mungu kutoka 20 2-4 . Psalm 96:9, Psalm 29:2 Tunapomwabudu mungu naye Mungu hufurahiwa na sisi Zephaniah 3:17 Rom 12:1-2

Your Worship = Your View of God
jinsi unavyoabudu ndiyo mwonekano wa mungu ulivyo ndani yako, haijarishi unaabudu wapi uwe peke yako au mko wengi kama unaabudu kwa kutokumaanisha au kumaanisha itajulikana tu na hivyo ndivyo mtu anaweza kujua ni jinsi gani mtazamo wako kwa Mungu wako.

KUNA NGUVU KATIKA KUSIFU NA KUABUDU
Yoshua 6:20 Matendo 16:23-26 zinaonyesha ambavyo kwa kutumia kusifu tu Mungu alishuka na kufanya lile lililokuwa hitaji lao.

Kusifu kunamfukuza adui
Psalms 50:23. 2 Nyak 20:22. Ukiwa unasifu na kuabudu humfukuza adui mbali kutokana na ukiwa kwenye ibada Mungu hushuka maana yeye anasema anakaa katikati ya sifa hivyo palipo na Mungu shetani hawezi kuwepo lazima akae mbali.akimbie mbali kabisa maana kunakuwepo na uwepo wa bwana wa Majeshi.

Je, ni wakati gani tuabudu?
Ni niyakati zote zinafaa kumwabudu Mungu. Kwa nyakati zilizotengwa Zaburi ya 100 inatuelekeza namna ya kuanza, lakini zaidi ya yote tunapaswa kuishi maisha ya ibada bila kukoma. Kwa kila tunapopumua, kwa kila wazo, kwa neno na tendo, tunapaswa kumwabudu Mungu wetu mzuri tunayemtumikia milele na milele Zab 145:1,2

mwa 12:6- Siku zilipita na watu wakafanyia ibada kwenye Hekalu na kwenye masinagogi; lakini siku hizi miili yetu ni hekalu la Mungu 1Kor 6:19 tu hekalu la Mungu sisi ibada zinatakiwa zifanyike kila wakati na si mara moja kwa wiki kama wengine wanavyo dhani.

Je, Tunafanyaje Ibada?
Biblia inatufahamisha jinsi watu walivyotumia mioyo yao, mawazo yao, mikono yao, viganja vyao, miguu yao, na midomo yao katika uimbaji. Walipaza sauti zao kwa furaha na kusujudu, kucheza, kusifu, kubariki na kushukuru.

Maneno kama halal na haleluya kutoka katika Zaburi yana maana ya kusifu, kumwinua na kumwadhimisha Bwana. Neno Yadah lina maana ya kunyoosha mikono hewani, na neno barak lina maana ya kupiga magoti katika ibada ya kumbariki Mungu. Kuitoa miili yetu katika kumhudumia Mungu na mwanadamu ni ibada pia (Rum 12:1). Watu pia humwabudu Mungu katika sanaa zao, katika uandishi wao, katika michezo ya kuigiza, katika muziki, katika usanifu wa majengo, na hata katika utoaji wa fedha zao kwa ajili ya Injili.

Kusifu na kuabudu sio kuimba tu
Watu wengi wanajua kuwa kusifu na kuabudu ni kuimba tu hapana kuna njia nyingi za kusifu au kuabudu, unaweza kutumia sanaa nyingine kumwabudu mungu au watu wengine wakamwabudu Mungu mf maigizo, ngonjera, shaili, uchoraji, upambaji au unakshi wa vitu, kujenga .nk

Ibada Kanisani
KatIka kanisa makusanyiko yetu yanapaswa kujawa na zaburi, nyimbo, na tenzi za rohoni ambazo zinaweza kuongozwa na Roho katika lugha mpya anazotupatia Yeye. Kwahiyo mikutano mingi ya kisasa haina tofauti sana na burudani za kikristo kama kwenye kumbi za starehe. Watu huwa wanaangalia tu, lakini je, wanaabudu? Uwepo wa Mungu na Roho wake katika ibada zetu utawafanya watu wasioamini kuanguka chini na kuabudu (Kol 3:16) (1Kor 14:15,16,25,26) (Efe 5:19) (Mdo 2:4).

Ibada Ya Kweli Ina Gharama
Biblia inazungumzia habari za sadaka za kusifu. Daudi alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote, na akakataa kumtolea Mungu kafara ambayo isingemgharimu cho chote (2Sam 6:14; 24:24). Wale mamajusi wa Mashariki walitoa zawadi za gharama kubwa walipokuja kumwabudu Yesu (Mt 2:9-12), na mwanamke mmoja alimpaka Yesu kwa mafuta ya gharama kubwa, akamwosha miguu yake kwa machozi yake, na kuifuta kwa nywele zake (Lk 7:36-50). Hivyo ibada yoyote inaambatana na kutoa tena vitu vyetu vya thamani.

Tunapaswa kumsifu Mungu kwa jinsi alivyo na kwa matendo yake; lakini Mungu mwenyewe anawatafuta na anawataka wafanya ibada, na si mradi ibada tu. Kusifu kwaweza kufanywa hadharani, lakini ibada mara zote ni jambo la ndani ya moyo. Kusifu mara zote kunaweza kuonekana au kusikika, lakini kuabudu yaweza kuwa ya kimyakimya na iliyofichika. Kusifu kunaonekana, kuna kutumia nguvu, kuna misisimko na furaha; lakini ibada mara zote ni heshima na hofu katika uwepo wa Mungu.
Biblia pekee inatuonesha jinsi Mungu anavyo hitaji na kutamani kuabudiwa na yeye pekee yake ndiyo anayestahili kuabudiwa.

Kusifu na kuabudu kwa siku za leo
Katika siku za leo kuna ufinyu wa mafundisho katika kusifu na kuabudu na ndiyo maana ya kuanda somo hili ili tupanuane mawazo. Watu wengi wa leo wanadhani kusifu ni kuimba kwa nyimbo zenye midundo ya harakaharaka(zouk&sebene) na ukipunguza spidi ndo kuabudu. Hasha tunaposema kusifu inatokana na maneno yaliyopon kwenye wimbo husika kweli ni ya kusifu, kama ni maneno ya kusifu tunasema ni wimbo wa sifa haijarishi speed inayotumika na hali kadhalika nyimbo za kuabudu. Watu katika kipengele hiki huwa wanachakanya nyimbo utakuta wakati wa kusifu anaimba wimbo wa kutia moyo au wa maombi, kinachotakiwa ni kujua kuwa kila jambo lina wakati wake ziiko nyimbo za mazishi, kufariji, kutia moyo, za maombi, za kusifu , na za kuabudu nk sasa usichanganye kwenye kusifu wewe unaimba parapanda italia au tuonane paradiso, hizo sio za sifa sasa najua wewe utafanya zoezi la nyimbo unazozijua ili kufahamu zina ujumbe gani na ziko katika kundi lipi kati ya hayo niliyokufundisha hapo juu.

Baadhi ya maandiko yanayo onyesha aina za kusifu na kuabudu kwa:

1. Kusimama (Zab 135:1-2, 134:1)

2. Kuinua mikono (Zab 134:2, 28:2)

3. Kuinama au kupiga magoti (Zab 95:6)

4. Kupiga makofi (Zab 7:1)

5. Kucheza (Zab 149:3, 150:4, 2Sam 6:14)

6. Kicheko (Zab 126:2, Ayu 8:20-21)

7. Kufurahi (Kumb 12:11-12, Law 23:40)

8. Kutembea (2Nya 20:21-22)

9. Shangwe (Zab 95:1)

10. Kupiga kelele (Zab 66:1, Law 9:23-24)

11. Kupiga vigelegele (Zab 33:1, 32:11)

12. Ukimya (Mhu 3:7)

13. Kupaza sauti (Isaya 12: 6, Zab 42:4)

14. Kulia/ kutoa machozi katika roho mtakatifu

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa

Mpango Wa Mungu Kwa Ulimwengu


Katika Biblia Yako SomaIsaya 66; Zaburi 67.
Mstari wa Kukariri
 ‘
…wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia,”Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike,kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu,naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.” (Isa 41:9,10).
Baadaye Zungumzieni Jambo HiliMwambie mwenzako Msalaba unaweza kumaanisha nini kwako kwa kile ambacho Mungu anaweza kukitaka kwako; pengine atataka uende mahali fulani, au atakuamuru kufanya jambo fulani,  au atakuamuru kutoa kitu fulani, au atakuamuru kuacha jambo fulani.
Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana TenaKwa kuzingatia kwamba muda unakwenda mbio na siku ya mwisho inakaribia, hebu fanya maombi kwa upya ukimkabidhi Yesu wenye dhambi wawili kutoka kwenye familia yako au miongoni mwa rafiki zako.
Kazi ya Kuandika Ya StashahadaJe, unauhisi mkono wa Mungu ukiwa juu ya maisha yako ukikuchagua kumtumikia Yesu? Andika ukurasa mmoja wenye maelezo ya kile unachofikiri  Mungu anakuitia. Je, unafikiri anakuita uwe nani au ufanye nini?
Tafakari Mistari IfuatayoIsa 43:4-7
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea Falme za Kiarabu.
Wapo Waislam 2,200,000 katika majimbo 7; Kuna umaskini kwenye utajiri mkubwa Huduma ya Kikristo imekatazwa; Hakuna Kanisa nchini humo

Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.

Kwa kawaida tunapenda kuhusisha Agizo Kuu na maneno ya mwisho aliyoyasema Yesu katika Injili zote, na hasa Mt 28:16-20, na katika Matendo.
Katika kitabu cha Mwanzo, Baba Mungu aliyesalitiwa na kuhuzunishwa, anatembea bustanini wakati wa jua kupunga akiwatafuta rafiki zake, mwanamume na mwanamke; ambao muda mfupi tu uliopita wamepoteza imani yao, kwa kuamua kumtii Shetani na kusababisha madhara makubwa kwa ulimwengu. Maneno ya Baba yanaelezea upendo wake, ‘Adamu uko wapi?’ Na kwa swali hilo haielekei kama Mungu alikuwa anataka kujua alikokuwa amejificha Adamu! Biblia inatuonesha kwamba Mungu alianza kuweka mambo sawa kwa kutoa ahadi (Mwa 3:9).
Katika kitabu cha Mwanzo pia kuna habari za Yusufu, mtu aliyetumwa na Mungu kuokoa taifa (Mwa 37-50).
 
Katika kitabu cha Kutoka, Mungu anaonesha uwezo wake wa kuokoa taifa kutoka utumwani. Anataka kuwabariki kwa kuwafanya taifa la kimishenari kwa kulipeleka Neno lake na uzima wake kwa ulimwengu wote (Kut 3:7-19:6).
 
Katika Zaburi, Mungu ameuonesha upendo wake mara kwa mara (Zaburi 67, Zaburi 2, Zab 72:17).
 
Manabii na manabii wadogo kama Yona walijazwa na uwezo wa kimbingu, japo kwa vipindi vidogovidogo, wa kuupenda ulimwengu (Isa 6:1-8; Isa 54:1-5; Hab 2:14)..
Mpango wa Mungu kwa ulimwengu wote unadhihirishwa na Nabii Isaya anaposema kwamba kuna mambo manne anayokusudia Mungu kuyafanya; vilevile yapo mambo mawili ambayo Mungu anataka sisi tuyafanye (Isa 66:18-21).
1. Mungu anasema, ‘Ninakaribia Kuja’
Katika Isa 66:18, huu ni ufunuo wa kinabii kuhusu Kuja Mara Ya Pili kwa Kristo.  Wakati huo atawakusanya mataifa yote pamoja kutokana na vitendo vyao na hisia zao. Hakuyafanya hayo alipokuja mara ya kwanza. Tutalijadili hilo baadaye na kuona ishara duniani na katika Ufalme zinazoashiria kurudi kwa Yesu.
Maana yake ni kwamba ipo siku ya mwisho. Hizi ni habari njema kwa kila mwamini, lakini pia ina maana kwamba kuna siku ya mwisho kwa kila mmoja wetu kuwaleta kwa Yesu jamaa zetu, rafiki zetu, na mataifa.
2. Nitafanya Ishara Miongoni Mwao
Ishara katika Isa 66:19 ni Msalaba, na huu unajulikana ulimwengu mzima. Kwa asiyeamini, Msalaba ni tamko la dhahiri la upendo mkuu wa Mungu kwa ulimwengu wote (Yn 3:16) Lakini kwa kila aaminiye, Msalaba una maana kubwa zaidi. Kalvari ilianzia Gethsemane na Yesu katika ubinadamu wake Msalaba ulimaanisha mapambano ya:
Kwenda asikotaka kwenda,
Kufanya asichotaka kukifanya,
Kutoa asichotaka kukitoa.
(Mt 26:39) (Lk 9:23)
Hapakuwa na njia nyingine. Na kwa furaha iliyokuwa mbele yake, furaha ya kukuona wewe ukiwa salama mbinguni, Yesu aliuvumilia Msalaba. Sisi nasi yatupasa kuvumilia kwa ajili ya wengine (Ebr 12:2).
3. Nitawapeleka Katika Mataifa Baadhi ya Wale Waliopona
Mbali sana; Hispania, Libya, Asia, Ugriki,na baadhi ya visiwa (Isa 66:19). Leo hii watu wa makanisa ya mataifa yaliyoendelea wanafanana sana na watu wa ulimwengu na ambao hawajafikiwa na Injili. Kwa ajili ya hao Yesu ataita watu na kuwatuma mbali sana kama wamishenari.
Je, unapaswa kupona nini?
Unapona mateso ya Msalaba na hitaji lake la kifo na kufanya mapenzi ya Mungu kwa gharama zote (Lk 9:23).
 
Unaponaje?
Ni ajabu, unapona tu na kuokoa maisha yako kwa kukubali kupoteza maisha yako kwa ajili ya Yesu na mapenzi ya Mungu (Lk 9:24).
Sasa tutaangalia na kuona yale mambo mawili ambayo tunapaswa kuyafanya ikiwa ni mwitikio wetu kwa wito wa Mungu wa kutumwa. Mambo yenyewe si magumu sana.
4. Watautangaza Utukufu Wangu
Je, utukufu wa Mungu ni nini? Ni Mungu aishiye Mwenyewe. Tunatangaza uwepo wake, upendo wake, nguvu zake, uweza wake, huruma zake na neema yake. Tunamtangaza Mwanaye, maisha yake, kifo chake, kufufuka kwake, na kwamba yu hai leo na anaweza kuokoa, kusamehe, kuponya, kuweka huru, na kuwajaza watu na Roho wake. Na ndipo utukufu wake unakuwa dhahiri kwa maisha yaliyobadilishwa (Isa 66:19; Mdo 1:8).
5.Watawaleta Ndugu Zako Wote
Mara zote Injili itafanya kile kilichoahidiwa kwenye Injili, na mwitikio wa watu ni kumfuata Yesu (Isa 66:20; Yn 12:32). Tutawaleta hadi mlima wake mtakatifu-hili likimaanisha ufuasi miguuni pa Yesu, (k.m. Mt 5:1).
Je, waamini wapya watatoka wapi?
Watakuja wamepanda farasi - ikiwa na maana ya mataifa ambayo hayajafikiwa ya Asia ya Kati. Tangu mwanzo farasi wengi walitokea eneo hilo.

Watakuja wamepanda magari
- ikiwa na maana ya watu waliorudi nyuma kutoka mataifa ya Magharibi.

Watakuja wamepanda vihongo
– ikimaanisha watu kutoka mataifa yanayoendelea.

Watakuja wamepanda ngamia
– ikiwa na maana ya watu kutoka mataifa ya Kiarabu kwenye Uislamu.

6. Nitachagua Baadhi Kuwa Makuhani
Hatua ya mwisho ya ufunuo wa Nabii Isaya ipo katika mstari wa 21 (Isa 66:21).  Ni unabii ulio sahihi kabisa kuhusu mambo ambayo Mungu anayafanya sasa katika ulimwengu mzima. Anawaita wanaume na wanawake walioamua kumfuata Bwana, kutoka watu wa mataifa yote na tamaduni  zote, kuacha yote na kumfuata Yesu. Tunaweza kumwona mwamini mchanga akipambana ili kuwa huru na dhambi, lakini Yesu anaona uwezekano wa mwamini huyu kuwa mtu wa Mungu, na anamchagua kuhudumu (Mk 1:17).
Mordecai Ham ni Mwinjilisti Mmarekani ambaye hakujulikana sana; na katika kuhubiri kwake katika mji mmoja zamani sana, hakujua kwamba kijana mmoja aliyetoa maisha yake kwa Yesu jioni ile baadaye angekuwa mhubiri mkubwa akiwahubiria mamilioni ya watu kote ulimwenguni katika muda mrefu wa huduma yake. Je, wamfahamu kijana huyo? Alikuwa ni Billy Graham ambaye jioni ile Mungu alimchagua kwa makusudi yake matakatifu.

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu
Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili Ya Yesu Kristo

Burkina Faso
Jina la Watu
Lugha Yao
Idadi Yao
Djan (Dian, Dyan)
Dian
14,100
Seemogo
Sambla (Seeku)
17,000
Senabi (Niangolo)
Senoufo, Senar (Nyangola)
50,000
Syem (Karaboro, Western, Syer)
Karaboro, Western
19,500  

Wednesday, November 7, 2012

Prayer for Salvation


1 God Loves You!

The Bible says, "God so loved the world that He gave His one and only Son, that whoever believes in Him shall not perish, but have eternal life"
The problem is that . . .

2 All of us have done, said or thought things that are wrong. This is called sin, and our sins have separated us from God.

The Bible says “All have sinned and fall short of the glory of God.” God is perfect and holy, and our sins separate us from God forever. The Bible says “The wages of sin is death.”
The good news is that, about 2,000 years ago,

3 God sent His only Son Jesus Christ to die for our sins.

Jesus is the Son of God. He lived a sinless life and then died on the cross to pay the penalty for our sins. “God demonstrates His own love for us in that while we were yet sinners Christ died for us.”
Jesus rose from the dead and now He lives in heaven with God His Father. He offers us the gift of eternal life -- of living forever with Him in heaven if we accept Him as our Lord and Savior. Jesus said "I am the way, the truth, and the life. No one comes to the Father except by Me."
God reaches out in love to you and wants you to be His child. "As many as received Him, to them He gave the right to become children of God, even to those who believe on His name." You can choose to ask Jesus Christ to forgive your sins and come in to your life as your Lord and Savior.

4 If you want to accept Christ as your Savior and turn from your sins, you can ask Him to be your Savior and Lord by praying a prayer like this:

"Lord Jesus, I believe you are the Son of God. Thank you for dying on the cross for my sins.  Please forgive my sins and give me the gift of eternal life.  I ask you in to my life and heart to be my Lord and Savior. I want to serve you always."

Did you pray this prayer?

YES NO

Je inamaanisha nini kuwa Mungu ni upendo? Je inamaanisha nini kuwa Mungu ni upendo?

Swali: "Je inamaanisha nini kuwa Mungu ni upendo?"

Jibu:
Hebu tuweze kuangalia vile Bibilia inaelezea upendo, na kisha baadaye tutaangalia namna chache vile Mungu ni sehemu kuu ya upendo. “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabiri; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote” (1Wakorintho 13:4-8a).Hii ndilo elezo la juu sana la Mungu kuhusu upendo, na kwa sababu Mungu ni upendo (1Yohana 4:8) hivi ndivyo ilivyo.

Upendo (Mungu) hajilazimishi/haujilazimishi kwa mtu yeyote. Wale wanaokuja kwake wanafanya hivyo kwa kuitikia upendo wake. Upendo (Mungu) huonyesha upole kwa watu wote. Upendo (Yesu) alizunguka kote akifanya mazuri kwa watu wote bila upendeleo. Upendo (Yesu) hakutamani kitu cha wengine walikuwa nacho, aliishi maisha ya unyenyekevu bila kunung’unika. Upendo (Yesu) hakujivunia vile alivyo kuwa kimimwili, ingawa aliweza kumshinda nguvu kila mtu aliyekutana naye. Upendo (Mungu) haulazimishi unyenyekevu. Mungu hakulazimisha Mwnawe kunyenyekea, lakini kwa mubadala Yesu kwa pendo lake alimtii Babaye wa mbunguni. “Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu” (Yohana Mtakatifu 14:31). Upendo (Yesu) alitwaza/na huwaza yaliyo mazuri kwa matakwa ya wengine.

Tibitisho kuu la upendo wa Mungu limeelezwa kwetu sisi katika Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Warumi 5:8 yakiri ujumbe sawa na wa Yohana: “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” Tunaweza kuona kutoka aya hizi kuwa nia kuu ya Mungu ni tuwe pamoja naye katika mji wake wa milele, mbinguni. Ameifanya njia rahisi kwa kulipa gharama ya dhambi zetu. Anatupenda kwa sababu alichagua kwa kutekeleza kifungu cha nia yake. Upendo husemehe. “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” (1Yohana 1:9).

Je inamaanisha nini Mungu ni upendo? Upendo ni sehemu kuu ya Mungu. Upendo ni sehemu kuu ya tabia ya Mungu, na utu wake. Upendo wa Mungu kwa vyovyote vile haugongani/hitilafiana na utukufu wake, utakatifu na haki yake hata gadhabu yake. Sehemu zote za Mungu kwa pamoja zimekamilika. Chochote Mungu anatenda hupendeza, haki kwa sababu kila afanyacho hukifanya kwa haki na usawa. Mungu ni mfano mtakatifu wa upendo wa kweli. Cha kushangaza, Mungu amewapa uwezo wa kupenda vile anavyo penda, kupitia nguvu za Roho Mtakatifu wale wote watakaomkubali Mwanawe kama mwokozi wa maisha yao. (Yohana 1:12; 1Yohana 3:1, 23-24).

Wednesday, October 10, 2012

MAKOSA WANAYOFANYA VIJANA KATIKA KUTAFUTA MWENZI WA MAISHA.

KWA NINI VIJANA WENGI WANAKOSEA KATIKA KUTAFUTA MWENZI WA MAISHA?
Maamuzi ya kuoa au kuolewa, si maamuzi madogo, ni moja ya maamuzi makubwa ambayo vijana wengi wa kike na wa kiume wana kutana nayo kila siku. Sasa katika kufanya maamuzi haya ukweli ni kwamba sehemu kubwa ya vijana mpaka wafike mahali pa kumpata kijana au binti wa kusema huyu ndiye haswa wa kutoka kwa Bwana, basi ujue tayari wengi wanakuwa walishakosea mara nyingi mpaka kufikia hapo. Wapo ambao wakikosea husema, yule wa kwanza hakuwa chaguo la Bwana, au haukua ufunuo wa Mungu mwenyewe bali malaika, au utasikia mwingine akisema Bwana amemchukia Esau akampenda Yakobo au amehamishia upako wa Sauli kwa Daudi kwa maana ya kwamba upako umehama kutoka binti wa kwanza hadi kwa mwingine. Mimi sina uhakika sana na hizi kauli.
Je hivi kweli hayo ndiyo yalivyo au ni ujanja ujanja tu wa vijana tena hasa wa kiume ndio wenye kauli kama hizi. Lengo la waraka huu mfupi kwako kijana mwenzangu ni kutaka kukueleza sababu kadhaa ambazo kupelekea vijana wengi kufanya makosa katika kutafuta mwenzi wa maisha.
*Wengi wanakuwa tayari wameshafanya maamuzi ya nani ataishi naye.Vijana wengi huwa wanaomba Mungu awape mtu sahihi wa kuishi naye na wakati huohuo tayari kwenye nafsi yake anakuwa na mtu wake kwamba lazima huyu tu ndiye nitaishi naye. Na kwa sababu hiyo ina kuwa ni vigumu kwao kumpata mtu wa mapenzi ya Mungu na pia ina muwia kazi Mungu kukuonyesha mke au mme wa kusudi lake kwani tayari umeshafanya maamzi ndani yako, je Mungu afanye nini kama sio kunyamaza.
*Sababu za kipepo
Hapa nitaelezea mambo mawili kwa wakati mmoja, la kwanza ni hili kuna vijana huenda wao wenyewe au ndugu zake, wazazi wake walishawahi kumtoa huyo mototo kama dhabihu kwa mapepo kwa sababu ya mila zao au pia alipatikana kwa njia za kipepo. Siri moja ni hii kuna baadhi ya mapepo huwa hayapendi kushare sex na mtu mwingine, hivyo ni lazima yalete kila namna ya upinzani ili mtu asiolewe na wala kuoa. Na mwingine hata kama hakutolewa kama dhabihu lakini huenda pepo wameshawahi kufanya mapenzi na huyo mtu na kama yatampenda basi ujue hayatakubali aolewe au kuoa, hivyo yatamletea kila namna ya upinzani katika kuolewa au kuoa kwake. Mengine hufika mahali hata pa kumwachia kijana wa watu harufu mbaya ili mwingine asimpende.
*Maneno ya kujitamkia
Kuna baadhi na hasa hapa ni akina dada kwa sababu mbalimbali kama vile kubakwa, kujeruhiwa katika nafsi kwa sababu ya kuachwa na mchumba wake hufikia mahali wakasema mimi sitaki tena kuolewa. Sasa inpofika muda umepita na wanataka tena kuolewa wananaza kuomba Mungu awape mume, wakati huo wamesahau kwamba walishatamka kwamba hawataki tena kuolewa. Nisikilize ukisema hutaki kuolewa au kuoa tena, maana yake unaifunga nafsi yako hapo kwamba hutaoa kuolewa, na Biblia inasema mtu atashiba matunda ya kinywa chake. Na wakati huo shetani ni mwepesi kufuatilia maneno ambayo ni ya athari kwako. Sasa bila kufuta kwa Damu ya Yesu ndugu utakesha hapo.
*Dhambi.
Sikiliza Biblia inasema afichaye dhambi zake hatafanikiwa, (Mithali 28:13a). Kuna baadhi ya vijana huwa wanakuwa awali kuna baadhi ya dhambi wamezifanya na hawajazitubia, na bado wana taka mtu awaoe au wa kumwoa. Biblia iko very clear kama kuna dhambi umeficha hutafanikiwa, sasa inategemeana, lakini pia inahusiana sana na kutofanikiwa kwako pia kumpata hata mwenzi tu. Nikupe mfano mara nyingi watu wanatoa mimba, au watoto wanaozaa, nao pia kupata mume au mke huwa inakuwa kazi kweli kweli.
*Kutokuenenda kwa Roho.Paulo anasema, “Basi nasema enendeni kwa roho wala hamtatimiza kamwe tama za mwili” (Wagalatia 5: 16). Kuenenda wa Roho maana yake ni kuongozwa na Roho Mtakatifu, hii ni pamoja na zoezi zima la kutafuta mke au mme. Sasa kwa sababu wewe unaenda kwa mwili, mara eti nataka mtoto portable, mguu wa chupa, mweupeee, nk. Hivyo vitu unavyotaka wewe kuna wengine pia wanataka hivyohivyo na matokeo yake mnaanza kugombaniana msichana au mvulana kwa sababu tamaa za miili yetu zinawaongoza huko.
*Kuwa na vigezo binafsi.
 Vijana wengi sana katika suala zima la kupata mke ua mme, ukweli wengi wao wana vigezo vingi sana ambavyo kila mmoja angependa huyo mchumba wake awe navyo. Utasikia lazima awe wa kabila ya kwangu, awe portable, mweupee, mrefu ndio mzuri, ajue kutabasamu na kisha awe ana ulamba. Sawa mi sikatai hivyo vigezo, lakini nikuulize swali Je! Unayajua mawazo ya Mungu kuhusu wewe kwa habari ya mkeo au mmeo? Je kibiblia hivyo vigezo vyako vinakubalika/ na je mke/mme mtu huchagua mwenyewe au hupewa na Bwana?
 Najua utaniambia mimi nitaomba Mungu anipe mke/mme mwenye sifa hizo. Ok. Ukiniambia hivyo na mimi nitakuambia kumuomba Mungu kwa muundo huo ni nzuri kabisa, wala sio dhambi lakini kumbuka maandalio ya moyo ni ya mwanadamu lakini jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana. Na hapo ndipo patamu, wengi huwa wanaomba kwa vigezo vyao, na mara nyingi Mungu anapojibu inakuwa tofauti na vigezo vyao, na hapo wengine wanakataa hata chaguo la Bwana wanabakia kuteseka. Jua kwamba wewe unapoweka vigezo vya mwenzi wako na Mungu naye ana vigezo vya aina ya mwenzi anayekufaa.
* Kufanya maamuzi kabla ya wakati.
Biblia inasema katika Mhubiri 3:1 “kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu”.Hili ni jambo la kawaida, hata wakati wa uchaguzi kura mtu harusiwi kupiga kama hajafikisha miaka kumi na nane kwa nchi nyingi. Vivyo hivyo hata suala la kutafuta mke au mume lina wakati wake maalumu. Ukitaka kulifanya nje ya kipindi ambacho Mungu amekipanga kwa ajili yako utateseka hadi uchoke. Kumbuka kila mtu ana muda wake, hivyo basi hakuna muda maalumu wa kila mtu kuanza kutafuta mke au mme, bali kila mtu ana muda wake na mara tu unapowadia Mungu humjulisha mtu wake.
Nisikilize ukiulekeza moyo wako upate kujua haya nisemayo na ukajizuia kufanya makosa kama haya, basi nataka nikuhakikishe suala la kupata mke au mme wa kutoka kwa Bwana litakuwa ni jepesi sana,ni sawa sawa na kuombea chakula na ukishafumbua macho ukaanza kula moja kwa moja ukiwa na uhakika kimeponywa na kubarikiwa.
Ndimi katika huduma hii,
Meshack.E.Kitova

MAMBO YA KUFANYA/KUZINGATIA KATIKA KIPINDI CHA UCHUMBA

Katika kitabu cha Muhubiri 3:1 Biblia inasema “Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”. Hivyo mwanadamu katika maisha yake hapa chini ya jua  kuna vipindi mbalimbali anavyovipitia hii ni pamoja na kipindi cha uchumba kwa sehemu kubwa ya watu.  
Katika kipindi hiki yapo mambo mengi ambayo wachumba hufanya, mengine ni mazuri na mengine hayafai kabisa. Na hii yote inatokana hasa na mitazamo au tafsiri ya uchumba kwa watu husika. Fahamu kwamba tafsiri unayokuwa nayo juu ya mchumba wako ndiyo inayokuongoza kujenga mahusiano ya aina fulani pamoja naye.
Lengo la somo hili ni;
Kuongeza ufahamu wa wachumba kuhusu kipindi hiki na Kuwapa vijana maarifa ya kuwasaidia kuishi kwa nidhamu ya Ki-Mungu katika uchumba wao. Pia ni kuwafikirisha vijana wanaotarajia kupita katika kipindi hiki mambo ya kuzingatia. Si wachumba wengi wanajua, Mungu anawataka wafanye nini katika uchumba wao au kwa lugha nyingine si wachumba wote wanaojua kwa nini kipindi cha uchumba kipo. Naam katika somo hili tumeandika mambo hayo kinaga ubaga.
Kwa kuwa suala la uchumba ni pana na lina mitazamo mingi, yafuatayo ni mambo tuliyozingatia katika uandishi wa somo hili;
  • Kuna makundi mbalimbali ambayo yana taratibu zao kuhusu mchakato wa mtu kumpata mke au mume kikiwepo kipindi cha uchumba. Makundi hayo ni pamoja na makanisa, makabila, familia nk.
  • Wachumba wanaweza kutofautiana kwa kiwango cha elimu, uchumi, ufahamu juu ya mambo mbalimbali, kikabila, umri na hata kwa rangi pia.
  • Kuna baadhi ya wachumba hadi kufikia muda wanakubaliana kwamba watakuja kuishi pamoja walishafahamiana tangu zamani na wengine hawakufahamiana.
  • Wachumba wanaweza wakatoka katika madhehebu/makanisa tofauti na hili ni kwa kuzingatia madhehebu/makanisa mengi yaliyopo.
Lengo letu ni kuandika juu ya mwongozo wa Neno la Mungu katika kipindi cha uchumba. kwa lugha nyingine, je Mungu anataka wachumba wafanye nini katika kipindi chao cha uchumba?. Kumbuka uchumba ni kipindi/wakati. Basi kama ni wakati jua kabisa kuna baadhi ya mambo ambayo ni lazima yafanyike, kwani Biblia inasema katika Mhubiri 8:5b “ Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu”, neno hukumu linamaanisha maamuzi, mambo ya kufanya.  
Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba;
Jambo la kwanza –  Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu
2Wakorinto 3:17 ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’.
Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya.
Kumbuka Paulo katika 2Wakorinto 12:9-10. —‘Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ….kwa hiyo napendezwa na udhaifu——- maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. Hivyo Roho Mtakatifu atabadilisha tafsiri ndani yako za vyote unavyoona kwa mwenzako huenda juu ya umbile lake, umri wake, macho yake, kabila lake viwe vitu vya wewe kujivunia. Zaidi Roho Mtakatifu pia atakuongoza katika maombi yatakayosidia kuuondoa ule udhaifu ambao umekuja si katika mapenzi ya Mungu, yaani wa kishetani.
Jambo la pilini wakati wa kuweka msingi imara wa uchumba wenu na kufahamiana zaidi.
Hili jambo ni la muhimu  kuzingatia. Ni vema wachumba wakatafsiri na kuelewa vizuri maana ya uchumba. Wachumba wanapaswa kuwa na mipaka fulani katika uchumba wao na  kuwa makini kwa kujilinda na mazingira ya kila namna ambayo yanaweza yakapelekea wao kuanguka dhambini. Ni vema mkajua kwamba ninyi ni wachumba na si wanandoa. Na kama ni wachumba basi uchumba una mipaka yake na hamruhusiwi kufanya mambo ya wanandoa. Mipaka hii iwe kwa habari ya kutembeleana,kupeana zawadi, mawasiliano (ingawa mnapaswa kuwa makini na lugha mnazotumia pia) nk.  Lengo la kutafsiri misingi ya mahusiano yenu ni kujiwekea mipaka na mazingira yatakayowasaidia kuishi maisha ya nidhamu, ushuhuda na kumletea Mungu utukufu.
Sambamba na hili sehemu kubwa ya wachumba huwa wanakuwa hawafamiani vizuri. Japo wapo baadhi ambao walianza tangu shule za msingi/sekondari/chuo na sasa wamechumbiana hivyo kwa sehemu wanafahamiana vema. Kwa wale wasiofahamiana vema huu  ni wakati wa kumjua mwenzako vizuri kwa maana ya kabila lake, familia yake, umri wake, interest zake, matatizo aliyo nayo yeye binafsi au ya kifamilia, mitazamo yake juu ya mambo mbalimbali kama uchumba, ndoa, maisha, wokovu, neno la Mungu nk. Huu ni wakati wa kumjua mwenzako kwa njia ya maswali mbalimbali ya msingi yanayohusu vitu nilivyovitaja hapo juu. Lengo hapa ni kujua mapungufu/madhaifu(weakness) na mazuri(Strength) za mwenzako ili mjue namna ya kukabilana na mapungufu na namna ya kuendeleza yaliyo mazuri.
Ni vema pia kuulizana historia zenu za maisha ya nyuma. Kabla ya kuokoka umepitia katika mifumo gani ya maisha ambayo imechangia kukufanya uwe ulivyo. Kabla ya kumpata uliye mpata ulikuwa umefuatwa na wangapi na uliwakubalia au la, na kama uliwakubali kwa nini mliachana, na sasa wako wapi, je bado wanakufuatilia. Hii itawasaidia sana kujipanga vizuri kimaombi na katika mahusiano yenu na zaidi itawasaidia kuweza kuchukuliana na kuhifadhiana katika madhaifu ya kila mmoja.
Mungu anapowaunganisha anakuwa na kusudi maalum. Hivyo jua kwamba huyo mwenzi uliyepewa umepewa kwa ajili ya kusudi fulani la Mungu. Ni wachumba wachache sana ambao pindi wanapokutana kila mmoja anakuwa anajua walau kwa sehemu kwa nini aliumbwa. Sasa ni vema mkae chini mfikiri, nini Mungu anataka kukifanya duniani kupitia ninyi? Na zaidi angalieni kazi zenu au yale mnayoyasomea, Je mtawezaje kuliimarisha agano la Bwana kwa pamoja kama mke na mume?.
Hapa maana yetu mnatakiwa kujibu maswali yafuatayo? Je ni kwa nini mlizaliwa? Je kwa nini Mungu amekuunganisha na huyo uliye naye sasa? Na je kupitia elimu, bisahara zenu au kazi mlizonazo mtawezaje kuimarisha agano la Bwana?, Kwa kuzingatia vipawa na uwezo Mungu aliowapa, je ni wapi Mungu anataka kuwapeleka na kuwafikisha? Kama ndani yenu mna huduma fulani, je ni watu gani ambao Mungu atataka mshirikiane nao katika huduma hiyo?, je ipi ni nafasi yenu katika mwili wa Kristo na taifa kwa ujumla? Ni vema zaidi mwanaume akajua wito/ kusudi aliloitiwa ili pia amshirikishe na mwenzake.
Kufanikiwa kwa hili kunahitaji uwepo muda wa kutosha wa wachumba kukutana ili kupanga na kuweka mambo yao mbalimbali, na kama ni watu walioko mbali basi suala la mawasiliano kwa njia mbalimbali kama simu, barua pepe, na barua na hata zawadi ni la muhimu.
Jambo la tatu- ni wakati wa kulinda wazo la Mungu hadi litimie.
Siku zote uamuzi wowote unaoufanya una gharama. Naam uchumba pia una gharama nyingi Sana za kuzikabili kuliko unavyofikiri. Gharama hizo ni pamoja na muda, pesa, mawasiliano, maombi, uhuru nk. Kumpata mchumba au mwenzi ambaye ni wa kusudi la Mungu, usidhanie ndio umemaliza. Kama huo uchumba wenu ni wa mapenzi ya Mungu muwe na hakika mtakutana na vita kubwa sana katika kipindi hicho cha uchumba na lengo ni kuwatenganisha. Ni lazima mjifunze siku zote kuombeana kwa kumaanisha maana Shetani naye yupo kazini ili kuvuruga hayo mahusiano.
Kumbuka huyo mwenzi ni agano toka kwa Bwana hivyo unawajibika kumlinda, kumlinda ni pamoja na kuhakikisha wewe hausabibishi au haufanyiki chanzo cha ninyi wawili kuanguka dhambini, au ukamwacha na kumsababishia majeraha ya nafsini na hivyo kuharibu mahusiano yake na Mungu. Wapo watu waliofikia kuharibu mahusiano yao na Mungu kisa mchumba, saa ya ibada imefika mchumba anasema twende zetu out bwana, unataka kufanya maombi ya kufunga mchumba anasema kesho nitakutoa out, inagharimu sana muda wa kuwaza pia kwa ajili yake na familia yake au mahitaji mbalimbali aliyo nayo.
Zaidi pia uchumba unaweza kukunyima uhuru hata wa kuwa na maongezi na rafiki zako, maana kuna baadhi ya watu huwa hawataki kuona mchumba wake anaongea au kucheka na watu wengine, na pia kuna wengine ni wachumba lakini wamewekeana taratibu ngumu utafikiri wanandoa kabisa na ukweli zinawatesa ila kwa sababu hataki kumpoteza huyo mchumba wake inabidi avumilie.  Jambo tunalosisitiza hapa ni kwamba, uchumba una gharama nyingi angalia mahusiano yako na Mungu yasiharibikie hapa.
Jambo la nne- ni wakati wa kupanga malengo na mikakati yenu ya baadae.
Mithali 29:18a “Pasipo maono, watu huacha kujizuia’
Hili si jambo ambalo vijana wengi hulipa kipaumbele linavyostahili. Katika hili ni vema wachumba wafikirie mapema ni aina gani ya maisha ambayo wangependa kuwa nayo, na pia je ni aina gani ya ndoa wanataka kufunga, tatu je ni wapi wangependa kuja kuishi kwa maishayaoyote. Haya yatawasaidia wahusika kujipanga ndani na nje kukabiliana na yaliyo mbeleyao.Kamawanataka kufunga harusi kanisani basi maana yake wanahitaji kuwa na maandalizi mazuri kifedha, waweke katika muda kila wanalotaka kuelekea katika harusiyaoili iwasaidie kujiaadaa mapema. Malengo yoyote yale ambayo mtaweka basi hakikisheni yanatekelezeka, yanafikika, yanapimika na mnayapangia muda wa utekelezaji.
Mambo zaidi ya kuzingatia katika malengo yenu;
Katika hili ni vizuri wachumba waangalie nafasi yao kifedha imekaaje, na changamoto zinazowakabili wote kwa pamoja. Je hali yao kifedha inawaruhusu kuzikabili gharama za maandalizi ya ndoa kwa ujumla. Je hali ya kimaisha ya kijana wa kiume inamruhusu wakati wowote baada ya kuchumbia aweze kufunga harusi kama anataka. Je nafasi zao kielimu zikoje, je kama zinatofautiana ni kwa kiwango gani? Na je tofauti zao kiuchumi na kitaaluma zinaweza kuwa kikwazo kwao kuoana, au kwa wazazi wao nk. Na je baada ya kuwa wamegundua na kupima uwezo wao katika hayo mambo mawili, je wanaweza wakasaidianaje ili wafike mahali pazuri wote wawili.
Vijana wengi wa kiume huwa wanakosea sana hapa, wengi huwa wanasema sitaki kuchumbia/kuoa mpaka niwe nimesha jikamilisha kiuchumi, niwe angalau na maisha mazuri. Sisi hatushauri sana dhana hii, ukweli ni muhimu kwa kijana wa kiume akjikamilisha kwa yale mambo ya msingi. Lakini fahamu kwamba kuna wakati mwingine kuendelea kwako kiuchumi, au kuvuka kwako kimaisha ni rahisi zaidi pale unapokuwa na mchumba au ndoa yako. Tunasisitiza tena ni vema wachumba wakae chini na kufikiri ni kwa namna gani wataendelezana kiuchumi na kitaaluma. Angalizo, ni vema uwe na uhakika kweli huyo mtu ni wa mapenzi ya Mungu kwa maana ya kuwa ni wa kwako kweli, maana wapo wachumba ambao wamekuwa wakisaidiana mpaka kulipiana ada, kupeana mitaji, kununuliana nyumba, magari nk, halafu mwishowe mmoja anavunja maagano, maumivu yake ni makubwa sana.
Jambo la tano – ni wakati wa matengenezo na kuzijenga nafsi zenu
Wachumba wengi huwa wanafichana mambo mengi sana wanapokuwa wachumba na matokeo yake hawayashughulikii mapema na hivyo yanakuja kuwaletea shida kwenye ndoa. Huenda kabla hujakubaliwa wewe tayari mwenzako alikuwa amesha wakubali vijana au mabinti wengine kwamba ataolewa nao au kuwaoa. Pia  kama ni msichana huenda ameshawahi kubakwa, au kutokana na masumbufu ya kupata mtu sahihi na wakati mwingine kuachika mara kwa mara imefika mahali huyo msichana akasema sitaki kuja tena kuolewa. Zaidi  huenda  mmoja wenu huko nyuma ameshawahi kufanya uasherati au zinaa kabla hamjachumbiana. Au kuna mwingine amekuwa akisumbuliwa na tatizo la harufu, kufanya tendo la ndoa na mapepo nk.
Haya yote na mengine mengi yanayofanana na haya yana athari kubwa sana kiroho na kimwili kwenu kama wachumba na wanandoa watarajiwa kama hayatashughulikiwa vema katika kipindi hiki cha uchumba. Licha ya kuwa na athari mambo hayo yamepelekea nafsi za watu au wachumba wengi kujeruhika. Nafsi inapojeruhiwa inaharibu ndani ya mtu mfumo wa kufanya maamuzi, mfumo wa utiifu kwa Mungu wake, mfumo wa kunia na kuhisi pia. Sasa mifumo hii inapoharibika inapelekea watu kufanya maamuzi ambayo yapo nje ya mapenzi ya Mungu kabisa. Nawajua baadhi yao ambao wameacha na wokovu, na, wengine wamekata tamaa ya kuolewa, wapo walioamua kuolewa na mataifa ilimradi ameolewa nk.
Hivyo basi tumieni wakati huu kufanya matengenezo na kujengana nafsi zenu kwa maana ya kuombeana sana, pili kwa kuongeza ufahamu wenu katika neno  la Kristo hasa maandiko yanayolenga uponyaji katika nafsi zenu, tatu kufuta na kufisha mapatano/maagano yote ambayo mmoja wenu aliyafanya huko nyuma na watu wengine na pia kufuta picha za kubakwa na kujenga ufahamu wa mtu aliyeathirika kisaikolojia kutokana na mambo kama hayo kwa njia ya Damu ya Yesu. Hatua hizi zitawasaidia kurejesha mifumo iliyoharibika na kuziruhusu nafsi zenu zifanye kazi kama inavyotakiwa.
Jambo la sita – ni wakati wa kujua taratibu mbalimbali kuelekea kwenye ndoa
Tumeshasema, kila dhehebu au kabila wana taratibu zao kuhusu uchumba hadi ndoa. Hivyo ni vema wachumba, wakafuata taratibu ambazo zimewekwa na makanisa yao hasa zile ambazo zipo katika mapenzi ya Mungu. Lakini pia lazima tukubali kwamba kuna baadhi ya taratibu za makanisa, makabila na hata madhehebu ambazo nyingine zipo tu lakini hazitekelezeki na nyingine hazimpendezi Mungu.
Sasa ni vema wachumba wazijue hizo taratibu na wajue je wanaweza kuzitekeleza au la, na kama hawawezi wafikirie kabisa wanafanyeje. Mfano kuna baadhi ya makanisa ambayo hayaruhusu mtu wa kwao aoe au kuolewa na mtu wa nje ya dhehebu hilo. Sasa hii ina maana kama una mchumba wa aina hiyo jipange kujibu maswali ya wazee wa kanisa na Mchungaji vizuri. Na zaidi kuna baadhi ya makabila na familia hazitaki uoe au kuolewa na watu nje ya kabila lako, au aliyekuzidi umri kama wewe ni kijana wa kiume nk. Hivyo ni vema kuzijua hizo taratibu ili mjue mnajipangaje kukabiliana nazo. Ushauri wetu ni huu kama una uhakika huyo mtu ni wa kutoka kwa Mungu basi simamia la Bwana maana lipi jema, kumpendeza Mungu au wanadamu?. Kumbuka Mungu ndiye mwenye ratiba ya kila mmoja wetu.
Suala la  kukagua/kupima afya zenu kwa pamoja.
Kwa mazingira ya ulimwengu wa sasa suala la ukimwi limechukua sura mpya na kuleta mtafaruku ndani ya kanisa hasa kwa vijana wanochumbia kabla ya kupima afya zao. Siku hizi jambo hili limewafanya wachungaji kuomba sana kwa habari ya vijana ndani ya kanisa. Sasa kama mlikuwa hamjapima afya zenu mpaka mmechumbiana basi chukueni hatua mwende kupima. Ni vema wachumba wakapima mapema afya zao ili jambo hili lisije likawaletea shida baadaye, maana kwa sheria ya nchi yetu wachungaji hawaruhusiwi kufungisha ndoa kama mmoja wa wahusika ameathirika.
Upimaji wa afya zenu ni wa muhimu kwani, ndani ya makanisa kuna rekodi ya vijana wengi tu ambao wameshaathirika na huenda si kwa sababu ya zinaa, maana kwa mujibu wa watu wa afya njia za maambukizi ni nyingi. Kuna wengine wamezaliwa nao, kwa nia ya kuongezewa damu,kutumia vifaa kama nyembe, sindano nk. Hata hivyo swali la msingi inabaki kwamba je, liko tumaini kwa mtu aliyeathirika kuoa au kuolewa?  
Tukueleze hivi, hakuna jambo gumu lolote la kumshinda Bwana, hii ni pamoja na ukimwi, kama Mungu alimfufua Lazaro, alitenganisha bahari ya Shamu na watu wakapita, kama Yesu alitembea juu ya maji, basi naomba ujue kwamba Ukimwi hauwezi kuzuia kusudi la Mungu hapa duniani kwa wale awapendao na kwa sababu hiyo tunasema hata kama mtu ana ukimwi na Mungu bado ana kazi naye hapa duniani, hakika atamponya huo ukimwi na atampa mke au mme.
Faida na lengo la kupima ni hili, hata kama majibu yatatoka mmoja ameathirika isiwe mwanzo wa ninyi kuachana. Kama mna uhakika Mungu aliwaanganisha huu ndio wakati wa kurudi mbele za Mungu kwa maombi ya uponyaji na kujipanga zaidi juu ya hilo.
Jambo la saba – ni wakati wa kuongeza ufahamu wenu kuhusu nafasi yako kwenye ndoa.
Je umeshawahi kujiuliza ni kwa nini Mungu anakupa mke au mme? Yamkini zipo sababu nyingi lakini baadhi yake ni; Mungu anakupa mke kama msaidizi, mlinzi, na pia unapopata mke au mme unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana na pia ni kwa sababu ya zinaa ndio maana unahitaji mwenzi. Hizi ni baadhi ya sababu zilizoko ndani ya Biblia. Hivyo basi tafuteni wanandoa mnaowaamini na zaidi waliokoka  muwaulize   kuhusu wajibu  wa kila mmoja kwa nafasi yake kwenye ndoa. Katika hili baadhi ya makanisa  huwa yana utaratibu wake wa nani atahusika na maelekezo ya aina hii kwa wachumba. Hivyo kama kanisa lako lina utaratibu huo, fuata huo utaratibu.
Katika ndoa kuna mambo mengi sana ambayo mtatakiwa kufanya, ni vema kufuata mwongozo na ushauri wa viongozi wenu au wachungaji wenu kuhusu nini mnatakiwa kufanya katika ndoa yenu. Angalizo hapa ni hili, uwe makini na vyanzo vya ushauri au mafunzo katika eneo hili ili lisije kuleta madhara baadae. Usitafute wala kufuata kila ushauri, bali sikiliza pia uongozi wa Mungu ndani yako.
Jambo la nane– Msifanye tendo la ndoa, maana jambo hili litaharibu mpango wa Mungu na kusudi lake kupitia ninyi.
Wakati wa uchumba, si wa kufanya mapenzi au kufanya michezo ya mapenzi. Tunarudia tena ili kuonyesha msisitizo kwamba chonde chonde jamani, uchumba sio ndoa, maana uchumba unaweza kuvunjika. Hairusiwi kabisa kwa wachumba kufanya mapenzi kwa maana ya tendo la ndoa kabla ya ndoa. Kitendo cha Mungu kukujulisha/kukupa huyo mwenzako kama mke/mume mtarajiwa haina maana mna haki ya kufanya mambo ya wanandoa. Mungu kukupa huyo mwenzako sasa ni taarifa kwamba  huyu ndugu ndiyo atakuwa mkeo au mmeo na anakupa taarifa sasa ili ujipange kufanya mambo ya msingi mnayotakiwa kuyafanya katika kipindi cha uchumba. Kipindi cha uchumba ndicho kipindi ambacho wachumba wengi sana wanavuruga kusudi la Mungu, na kuharibu maisha yao ya baadae na ndoa yao kwa ujumla.
Ndoa nyingi sasa hivi zina migogoro kwa sababu wakati wa uchumba walidiriki kufanya tendo la ndoa. Vijana wengi hawajajua kufanya tendo la ndoa kipindi cha uchumba lina madhara gani kwao na ndio maana wengine wanafanya. Biblia inasema katika Mithali 6:32 “Aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake mwenyewe”. Hata kama ukifanya tendo la ndoa na mchumba wako ambaye mlibakiza siku moja kufunga harusi, bado umezini.
Ndani ya nafsi ya mtu kuna akili, hisia, nia na maamuzi. Biblia inaposema afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake ana maana hii, dhambi hii inapofanywa, ina haribu mfumo wa utiifu na uamnifu kwa Mungu wako, inapelekea kukosa usikivu wa rohoni kabisa, ina haribu mfumo wa kufikiri, kunia na kufanya maamuzi. Na kwa sababu hiyo si rahisi tena kusikia na kutii uongozi wa Roho Mtakatifu. Kwa watu ambao wamezoea kuwa na mahusiano mazuri  na Mungu watanielewa ninachosema hapa.
Zaidi kuna baadhi ya wachumba kweli hawafanyi tendo la ndoa bali wanafanya michezo ya mapenzi. Michezo ya mapenzi (Fore play) ni maalum kwa ajili ya wanandoa, na ni sehemu ya tendo la ndoa. Hivyo kufanya michezo ya mapenzi ni kufanya mapenzi kwa sababu ile ni sehemu ya mapenzi. Kuna vitu unavichochea,  unaamusha hamu ya mapenzi au unayachochea mapenzi. Biblia inasema katika Mhubiri 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala  wa porini, msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vema yenyewe.”
Mungu pia anachukia michezo ya mapenzi soma Isaya 57:4-5 “Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani, juu ya nani mmepanua vinywa vyenu, Na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo; ninyi mnaowasha tamaa zenu kati ya mialoni, chini ya kila mti wenye majani mabichi….. Wachumba wengi hawajui haya kwa sababu si makanisa yote yanayofundisha maswala ya mahusiano ya wachumba kimpana.
Mpaka hapa tunaamini umeshajua hasara za jambo hili  na utazijizuia kabisa kulifanya. Michezo ya mapenzi ni pamoja na kunyonyana ndimi, kushikana sehemu ambazo zinaamsha ashiki ya mapenzi kama sehemu za siri, matiti, kiuno nk, pamoja na kuangalia picha za ngono. Katika kipindi ambacho tumemtumikia Mungu kupitia vijana tumejifunza na kukutana na kesi mbalimbali za aina hii na kuona namna Shetani anavyovuruga mpango wa Mungu kwa vijana. Mwenye sikio na asikie neno ambalo Roho wa Bwana awaambia vijana ili kulida kusudi la ndoa.
Ni imani yetu kwamba mambo haya nane yameongeza ufahamu na hivyo kuwa maarifa ya kutosha kukusaidia kuenenda kwa mapenzi ya Mungu katika kipindi cha uchumba.
Bwana awabariki

JIFUNZE KUFIKIRI KABLA HUJACHUKUA UAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA

Nawasalimu kwa jina la Yesu . Leo katika nyanja hii ya vijana, nimeona ni vema tukashirikishana kuhusu suala la ‘kufikiri kabla ya kuoa au kuolewa’.
Siku moja katika kusoma Biblia nilikutana na mstari ufuatao, nakushahuri uusome kwa umakini. Biblia katika 1Wakorinto 7:8-9 inasema “Lakini nawaambia wale, wasiooa bado na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo, lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa”.
Baada ya kuusoma mstari huu niliingia katika tafakuri nzito sana ambayo mwishowe ilinipeleka kuandaa somo hili, kwamba ni vema ukafikiri vizuri kabla ya kuchuka uamuzi wa kuoa au kuolewa.
Unajua malezi, dini, madhehebu yetu, wazazi, mila na desturi vinachangia kwa kiwango kikubwa sana kuhusu utaratibu wa kuanzia mtu kupata mke au mume mpaka watakapofunga ndoa. Kila kundi lina mfumo na utaratibu wake ambao lingependa vijana waufuate ili kuhakikisha wanaoa na kuolewa kwa kile ambacho kila kundi linaona na kuamini kwamba huo ndio uataratibu mzuri kufuatwa.
Namshukuru Mungu kwa kuwa nami nimeoa, ingawa vitu vingi sana Bwana alikuwa ananifundisha vinavyohusu ndoa hata kabla sijaoa. Nakubaliana na dhana kwamba ili uweze kuwa Mwalimu mzuri kwenye nyanja fulani basi ni lazima au ni vema wewe mwenyewe ukawa umepitia kwanza kwenye nyanja hiyo. Lengo ikiwa sio tu ufundishe ‘theory’ bali pia utufundishe na uzoefu wako binafsi kwenye eneo hilo. Licha ya kukubaliana na dhana hii, kwangu binafsi haikuwa hivyo, maana kuna mambo mengi ambayo, Bwana Yesu, alikuwa ananifundisha yanayohusu ndoa hata kabla sijaoa.
Kwa kifupi ndoa ni shule au darasa ambalo wanandoa wanatakiwa kukaa chini na kujifunza kila siku namna ya kuishi humo ndani ili kuweza kuishi maisha ambayo Mungu amewakusudia.
Kutokana na mifumo ya baadhi ya makanisa yetu, si vijana wengi ambao wanafundishwa kwa undani kuhusu maamuzi haya makubwa. Wengi wao wameingia kimwili na kujikuta wakijutia na kulaumu kwa nini nilimuoa au kuolewa na huyu kijana. Nasema haya kwa kuwa nimekutana na wanandoa wengi wa aina hii, na nataka nikuambie kama Biblia ingetoa mwanya wa wanandoa kuachana na kuoa au kuolewa na mtu mwingine, wapendwa wengi sana walioko kwenye ndoa wangefanya hivyo na wengine wasingekubali kuolewa au kuoa tena.
Unajua kwa nini?
Ni kwa sababu si vijana wengi wenye ufahamu wa kutosha juu ya aina ya maamuzi wanayotaka kuyachukua. Kwa hiyo katika somo hili nimeona vema niandike mambo manne ya msingi ambayo naamini yataongeza na kupanua ufahamu wako ili kukusaidia kufikiri kwanza kabla ya kufanya maamuzi haya makubwa;
  • Si kila ndoa inayofungwa imeunganishwa na Mungu, kwa kuwa ndoa ni kiungo cha muhimu kwa Mungu na Shetani pia.
Kuanzia mwaka 2005, Mungu alinipa kibali cha kuanza kufundisha na pia kushauri  juu ya mambo kadhaa kuhusu wanandoa. Tangu wakati huo hadi sasa nimekutana na baadhi ya wanandoa ambao wanajuta kwa nini walikubali kuoa au kuolewa. Wanaishi kwenye ndoa kwa sababu tu ya watoto na pia kwa hofu kwamba endapo kama wataachana jamii na watu wanaowazunguka hawatawaelewa.
Ni vizuri ukafahamu kwamba si kila ndoa inayofungwa ni ya mapenzi ya Mungu, hata kama imefungwa kanisani. Biblia inaposema kilichounganishwa na Mungu, mwanadamu asikitenganishe, katika nafasi ya kwanza maana yake iwe ndoa ambayo Mungu ndiyo aliyehusika katika kuanzisha mahusiano na kuwaongoza hao watu kuishi pamoja. Wakati Mungu anatafuta kuhakikisha watu wake wanaoana katika mapenzi yake na Shetani naye anapambana kuhakikisha watu wanaoana katika hila (mapenzi) zake.
Shetani amefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kuvuruga wanandoa wengi na kuwafanya waishi maisha tofauti na yale ambayo Mungu aliwakusudia. Ni kwa sababu hii ndio maana Paulo aliwaambia Wakorinto ‘Lakini nawaambia wale, wasiooa bado na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo, lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa’. Paulo aliona shida, maudhi ya wandugu walioko kwenye ndoa tokana na migogoro aliyokuwa akikutana nayo.
Fahamu kwamba ni furaha kubwa kwenye ufalme wa giza mtu anapooa au kuolewa kinyume cha mapenzi ya Mungu. Hii ni kwa sababu Shetani anajua akifanikiwa kukushawishi ukaoa kinyume na mapenzi ya Mungu, ameharibu ‘future’ yako na kile ambacho Mungu alikusudia ukifanye hapa duniani. Kumbuka suala sio kuoa au kuolewa tu, bali ni kuingia kwenye ndoa ambayo itakuwezesha kulitumika shauri la Bwana katika kizazi chako. Hivyo kabla hujaamua nani uishi naye hakikisha unamshirikisha Mungu akuongoze kumpata mwenzi sahihi.
  • Unapaswa kuoa au kulewa katika mapenzi ya Mungu
Naam kuoa au kuolewa katika mapenzi ya Mungu ni changamoto nyingine kubwa kwa vijana wa kizazi cha leo. Naam hili ni eneo ambalo Mungu yupo makini sana kufuatilia nani atakuwa mwenzi wako wa maisha. Na upande wa pili nao, Shetani anapigana kwa juhudi kubwa ili kuvuruga kusudi la Mungu kupitia mtu au watu.
Ni vizuri ukafahamu kwamba unapotaka kufanya maamuzi ya kutaka kuoa au kuolewa, Shetani naye ataleta mawazo (mapenzi) yake ndani yako juu ya nani anafaa zaidi  kuwa mwenzi wako maisha. Lengo lake ni kuhakikisha anakuunganisha na mtu ambaye anajua kwa huyo atakumaliza kiroho na kihuduma kabisa. Suala sio kuwazuia msiende kanisani, bali ni kuhakikisha kile ambacho ungefanya kwa kuwa na mtu sahihi hakifanikiwi. Ukitaka kujua ukweli wa jambo hili, muulize Mchungaji wako, kesi nyingi anazokutana nazo kanisani kwake zinahusu nini, naamini atakujibu kimapana. Ni jukumu lako kuwa makini kufuatilia unatii wazo la nani, Mungu au Shetani? 
  • Vigezo vya kimwili ni silaha kubwa ya uharibifu
Vigezo vya kimwili ni moja ya silaha kubwa ambazo Shetani anazitumia kuwavuruga watu wengi waweze kuoa au kuolewa nje ya mapenzi ya Mungu kwao. Jifunze kufukiri na kutafsiri mambo au makusudi kama Mungu anavyotazama na kutafsiri. Na uwezo wa kufanya hili utaupata kwenye neno lake tu. Kwako mwanaume Mungu anapokupa mke anakupa Mlinzi na msaidizi. Na kwa mwanamke Mungu anakuwa amekupa kichwa. Ni muhimu sana kuchunga ni msaidizi, mlinzi au kichwa gani unataka kiunganishwe na maisha yako kwa njia ya ndoa.
  • Ndoa ni wajibu mkubwa
Ndani ya ndoa kuna wajibu mkubwa sana unaokusubiri kama baba au mama. Ndani ya ndoa muda na uhuru wako unabanwa na mwenzi wako. Ndoa inabana pia muda wa kuwa na Mungu wako. Na kwa wengi kwa kutaka kuwapendeza zaidi waume au wake zao, wamefarakana na Mungu, kwa sababu wamewapa waume au wake zao hata nafasi na muda wa Mungu kwenye maisha yao.
Usiingie ndani ya ndoa kwa fikra za uapnde mmoja. Naam ndoa ni wito wa mapungufu na uvumilivu ambao ni lazima uwe tayari kuchukuliana na mwenzi wako katika mapungufu yake. Kuna vitu hamtaweza kufanana na kwa sababu ya mapungufu yaliyopo kwa kila mmoja  unapaswa kutafakari kuhusu majukumu yanayokuja kwako kama mwanandoa, hekima na busara katika kuzikabili changamoto za ndoa, kama vile kuzaa au kutokuzaa, kutokujiweza katika masuala ya unyumba, matumizi ya fedha, tabia za mwenzi wako nk.
Haya ni mambo ya kuhakikisha unayaombea mapema ili kujenga msingi imara utakapoingia kwenye ndoa yako. Lakini nikutie moyo kwamba endapo utaoa au kuolewa katika mapenzi ya Mungu, yeye ni mwaminifu, atakuunganisha na mtu ambaye katika changamoto mtakazokutana nazo hazitawakwamisha wala kuwafanya mjute. Bali endapo Shetani ndiye ataongoza maamuzi yako, ni majuto makubwa sana (asomaye na afahamu).
Mungu akubariki, naamini ujumbe huu umeongezea mambo ya kutafakari na kuzingatia kabla ya kufanya uamuzi wa kuoa au kuolewa.

KIJANA ZINGATIA HILI, ILI UWEZE KULITUMIKIA KUSUDI LA MUNGU. “Huu ni waraka maalumu kwa vijana wote ambao bado hawajaoa au kuolewa”.


Kijana mwenzangu ninakusalimu kwa jina la Bwana. Katika mwezi huu nina neno fupi ambalo nimeona ni vema nikushirikishe na wewe juu ya ‘UMUHIMU WA KUUTAFAKARI MWISHO WAKO UKIUHUSIANISHA NA KUSUDI LA MUNGU JUU YAKO’

Tarehe 26/04/2012 nilifanya maombi maaulumu yaliyolenga kuombea vijana ambao bado hawajaoa au kuolewa, nikimsihi Mungu afungue milango ya wao kuoa au kuolewa, kwa sababu wengi wao ninaowasiliana nao bado hawajaoa au kuolewa.

Katika kunijibu Mungu alinipa mistari kadhaa na kunifunulia tafsiri yake, nami nikaandika kwenye kumbukumbu zangu na mwezi huu nimeona ni vema na wewe nikushirikishe mafunuo haya maana naamini yatakusaidia;   

Fungu la kwanza ni, Luka 19:41 – 44.
Soma fungu hili lote, mimi nitanukuu maneno machache tu. “Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, akasema, laiti ungalijua hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani … siku zitakuja adui zako watakujengea boma … watakuangusha chini wewe na watoto wako … kwa sababu hukutambua  majira ya kujiwa kwako.

Fungu la pili ni, Isaya 1:2-3
“Sikieni enyi mbingu tega sikio ee nchi … kwa maana Bwana amenena; nimewalisha watoto na kuwalea nao  wameniasi, ng’ombe amjua Bwana wake, punda ajua kibanda cha Bwana wake, bali Israel hajui, watu wangu hawafikiri”.

Fungu la tatu (3) ni , Kumbukumbu  la Torati 39:29.
 “Laiti wangalikuwa na akili hata wakafahamu haya, ili watafakari mwisho wao”.

Katika mafungu haya matatu ya maandiko Roho mtakatifu alinifunulia yafuatayo;

*Kwanza alisema, usifikiri hao watu unaowaombea siwajibu. Wengi nilishawajibu, lakini wengine kwa sababu zao binafsi, wazazi wao, Viongozi wao n.k  hawajatii wazo langu juu yao/mapenzi yangu juu yao. Mimi ni Mungu ninayeangalia kesho/mwisho wa mtu/watu na lolote ninalofanya nimeliona mwisho wake. Sasa kwa kuwa hawa vijana wamekataa wazo langu kwa kutofikiria mwisho wao na kusudi langu kupitia wao na ndoa zao,  basi, hakika ndoa zao   zitakuwa na shida na baadhi yao wataniacha kabisa.

*Pili, Mungu kwa uchungu sana anataka mbingu na nchi zisikie na zijue kwamba   watoto wake ambao amewalisha na kulea  wamemuasi. Watoto hao wameshindwa kujifunza kupitia ng’ombe na punda, na tatizo lao ni kutokufikiri. Hii ina maana kutokufikiri kwao kumepelekea wao washindwe kumjua Mungu.  Kinamuuma sana Mungu, anapoona watu aliowaokoa na kuwafundisha au kuwaonyesha njia wapasayo kuiendea   wanakataa kwenda katika njia yake.

Zaburi 32:8 anasema “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, nitakushauri jicho langu likikutazama”. Sasa kitu kinachomuumiza ni pale anapowaonyesha watu njia yake au mapenzi yake kwao kuhusu wake/waume zao watarajiwa na akina nani halafu wao wanashindwa kutii. Licha ya kuwaonyesha au kuwajulisha mapenzi yake bado wameasi.


Ndugu kijana mwenzangu, natamani Mungu alete kitu hiki ndani yako kwa uzito ule ule aliouleta ndani yangu, ili usije ukakataa wazo la Mungu kwako na ukamkosea hata kuikosa mbingu kwa sababu tu ya mke au mume.

Sasa fanya yafuatayo ili kukaa katika mapenzi yake;

(a)   Jifunze kutafakari mwisho wako, ukijua ya kwamba mwisho wako uko mikononi mwa Mungu. Na kwa sababu hiyo maamuzi yoyote unayoyafanya ni lazima,  na si ombi umruhusu Mungu akuongoze ili uenende katika njia zake.
(b)   Haijalishi kwa jinsi ya mwili huyo mtu ana upugnufu/udhaifu wa aina gani kwa mtazamo wako, maadam una uhakika ni mtu wa mapenzi ya Mungu uishi naye, basi usijaribu kukataa huyo mtu kwa sababu Mungu ameona unakokwenda kukoje na huyo aliyemleta ndiye ambaye mtafika naye mwisho wenu.  
(c)    Hivyo basi wazo lolote/kijana/mtu yoyote anapokuja kwako kutaka   muoane na ndani yako unaona hakika ni mtu wa mapenzi ya Mungu, basi  kabla hujakataa kwa sababu zako binafsi, kaa chini utafakari, mhoji Mungu kwa maswali yanayokutatiza. Unapokwenda mbele za Mungu siku zote yeye ni mwaminifu atakupa majibu ya msingi na nina kuhakikishia unapotii uongozi wa Mungu kuna baraka za ajabu sana. Lakini unaposhindwa kutii  itakugharimu kuliko unavyofikiri.

  *Mungu anapokuonyesha/anapokupa mke au mme hamleti kwako kwa lengo la kukukomoa, bali anakua ameangalia kwanza kusudi lake, changamoto zilizopo mbele yenu na umbali mnaotakiwa kusafiri kwa pamoja kisha ndio anawaunganisha kwa kukupa mtu (mke au mume) ambaye anajua ukiwa naye hakika kusudi lake litafikiwa na mtaweza kuzikabili na kuzishinda changamoto zote zitakazojitokeza.

Hivyo mwenzi yoyote unayempata kama una hakika katoka kwa Mungu hata kama ana mapungufu gani kwa fikra zako au wazazi au dhehebu lako mimi nakushauri usimkatae, kwa sababu kwa huyo wewe utaweza kulitumikia shauri la Bwana.

Aliye na masikio na asikie lile ambalo Roho wa Bwana asema na vijana

KWA NINI ULIZALIWA AU KUUMBWA?

Mwanzo: 1:26“Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, WAKATAWALE samaki wa baharini na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi”
Katika waraka huu nataka tujifunze juu ya kusudi la wewe kuumbwa na nini ufanye ili uweze kutawala.    Zipo sababu nyingi za wewe kuumbwa lakini moja wapo na kubwa ni ili wewe uweze kutawala. Dhana ya  utawala ni pana, mimi nimeigawanya katika nyanja za kiroho, kidini, kisiasa, kiuchumi, ki-ardhi, kibiashara, ki-taaluma nk.
Sasa aina ya utawala ninayotaka kuzungumza ni utawala katika nyanja ya siasa inayopelekea utawala katika serikali. Yafuatayo ni mambo ya msingi ambayo yatakusaidia wewe uweze kutawala sawasawa na kusudi la Mungu la kukuumba;
(a)Kwanza amini kwamba wewe unaweza kuwa kiongozi mzuri na pia siku moja utakuja kuwa kiongozi mzuri  katika serikali ya nchi yako. Amini kwamba hauna upako wa kupiga kura tu, bali pia tayari Mungu ameshakupaka mafuta (upako) wa kupigiwa kura na wakati ukifika wapiga kura watathibitisha hilo.
(b) Pili, amini kwamba inawezekana kabisa kuokoka na wakati huohuo ukawa mwanasiasa na kiongozi mzuri wa taifa lako. Jifunze kutoka kwa wafalme mbalimbali katika Biblia kama vile Daudi, Yehoshfati nk. Siasa sio mchezo mchafu kama wengi wanavyofikiri, shida ipo kwa wale waliojiingiza kwenye siasa. Kama wanasiasa unawaona kama hawafai kwa kuwa ni waongo, au wala rushwa haina maana siasa ni mbaya.
(c)Fanya maamuzi ya kujiunga na chama chochote chenye sera nzuri katika nyanja zote za msingi na hasa kiuchumi. Nakushauri kabla hujajiunga na chama chochote, soma kwanza sera zao, uzielewe na kuzipima vizuri na kisha sasa amua kujiunga na chama hicho baada ya kuwa umeridhika na kuamini kwamba unaweza fanya nao kazi.
(d)Gombea kila aina ya uongozi katika chama chako kwa nafasi zake mbalimbali.
Kuanzia chini mpaka nafasi ya juu. Chukua fomu za uongozi, jaza bila kuwa na shaka, mwombe  Mungu akufanikishe, usiogope kushindwa katika uchaguzi, hayo ni matokeo na haina maana kwamba haufai, huenda sio wakati wa Bwana lakini pia kama kuna makosa uliyofanya jirekebishe
(e)Jenga mahusiano mazuri na makundi mengine katika jamii.
 Usiwabague watu kwa rangi, umri, kabila wala dini zao. Maana hao watu kwanza ndio utakaowaongoza ukipita, wao ndio watakaokupigia kura na zaidi baadhi
yao utafanya nao kazi katika ofisi moja.
(f)Mwisho ongeza ufahamu na Imani yako kuhusu siasa/uongozi. Nenda kwenye Biblia soma mistari yote inayohusu mambo ya utawala na uongozi ili uongozeke kiimani na pia zaidi ya hapo pia ongeza elimu ya dunia hii kuhusu mambo ya siasa.
Naamini ujumbe huu mfupi utakubadilisha kufikiri kwako kuhusu utawala (siasa) na kisha utayafuatilia mambo ya uongozi kwa karibu, hii ikiwa ni pamoja na kujiunga na chama chochote cha kisiasa hapa nchini.

KWA NINI TATIZO LA FEDHA LIMEKUWA SEHEMU YA MAISHA YA WAKRISTO?




Biblia imeshaweka wazi katika Yerema 29:11 na 3 yohana 1:2 kwamba mawazo aliyonayo Mungu juu yetu ni mawazo/mipango ya kutufanikisha, si hivyo tu bali anataka tufanikiwe katika mambo yote. Pia tunajua kwamba fedha na dhahabu ni mali ya Bwana si hivyo tu bali sehemu kubwa ya Biblia imejaa ahadi za Mungu za kutufanikisha kifedha na mafundisho mengi ya pesa.
Sasa licha ya haya yote na ukweli kwamba tumemwamini huyu Yesu lakini bado maisha ya mkristo mmoja mmoja, wakristo wengi, kanisa kwa ujumla, kwaya, makundi ya kiroho na huduma mbalimbali hali yake ya kifedha ni ngumu. Kila mtu analalamika juu ya pesa, mpaka imefika mahali tatizo la fedha limekuwa sehemu ya maisha.
Mikutano, semina tumeshindwa kufanya kisa fedha, vijana wameshindwa kuoa kisa pesa, kwaya hazirekodi kisa fedha. Kitu gani kimetokea kwa wakristo. Wazungu wanasema “Something must be wrong some where” maana yake lazima kuna kitu hakijakaa sawasawa mahali fulani.
Kusudi la waraka huu mfupi ni kukuelezea sababu ambazo zimepelekea tatizo la fedha kuwa sugu na kwa sehemu ya maisha kwa wakristo wengi. Sababu hizo ni ;
Moja, kukosa maarifa (mafundisho) ya kutumia fedha ki-Mungu. Hosea 4:6a Fedha ina kanuni zake za matumizi. Hivyo kushindwa kujua kanuni hizo na namna ya kuzitumia hizo fedha ki-mungu basi tatizo litaendelea kuwapo.
Mbili, matumizi ya fedha ya Mungu nje ya kusudi lake.
Hagai 2:8, Sikiliza fedha ni mali ya Bwana, hata ikiwa mikononi mwako bado ni ya Bwana, hivyo ni lazima itumike kwa mapenzi yake, maana kila pesa anayokupa ndani ina kusudi fulani au anakupa kwa lengo fulani.
Tatu, Roho ya mpinga kristo inafanya kazi ndani ya fedha.
 2 wathesalonike 2:7, sikiliza, shetani anajua ukiwa na fedha yeye atakuwa na hali ngumu sana maana utaituma hiyo fedha kuimarisha agano la Bwana, hivyo ameweka Roho ya mpinga kristo ndani ya fedha ila kupinga  fedha isiende kwa watu wa Mungu ili washindwe kumtumikia Mungu.
Nne, kukosa nidhamu katika matumizi ya fedha.
Tito 3:14 Watu wengi hasa waliokoka, hawana nidhamu katika matumizi ya fedha pindi inapofika katika mikono yao. Hawana malengo mazuri katika mtumizi ya fedha na kwa sababu hiyo wanajikuta fedha wanayoipata inatumika kienyeji na kwa sababu hiyo tatizo la fedha lina baki palepale.
Tano,Ufahamu mdogo wa Neno la Mungu kuhusu fedha.
 Wakristo wengi sana wanayo mistari mingi sana inayozungumza uponyaji na kutoa mapepo, na hata imani yao imeongezeka kwenye maeneo hayo. Lakini kwenye eneo la pesa ufahamu wao ni mdogo sana, si wengi wanaopata mafundisho katika nyanja ya fedha ya kutosha.
Sita, Kuwategemea wanadamu na si Mungu .Katika Yeremia 17:5 Mungu ametoa ole kwa wale wanaowategemea wanadamu.Hii pia imekuwa sababu kubwa sana ya tatizo la pesa kuwa sugu. Ni kweli watu wanamuomba Mungu awabariki, lakini mioyo yao inawategemea wanadamu na tayari ole imeshatiliwa kwa mtu anayemtegemea mwanadamu ki-mafanikio.
Mwisho, ni vifungo na laana za kifamilia, kiuokoo, kitaifa nk.
 Kwenye eneo la pesa, kuna baadhi ya watu wamefungwa wasifanikiwe kifedha katika ulimwengu wa kiroho. Hili ni tatizo la kiroho zaidi na pia wengine ni laana zinazotokana na kushindwa kulijua neno la Mungu. Soma kumbukumbu 28:15-60.
Ni maombi yangu kwamba Mungu akusaidie kuwa na mahusiano mazuri na yeye hasa kwenye eneo la fedha ili uone baraka zake

KWA NINI MUNGU ANATAKA WATU WAKE WAWE MATAJIRI?

Ile mwanzo 12:2 neno inasema “nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka”. Na Mwanzo 13:2 inasema“Naye Abramu alikuwa ni tajiri  kwa mifugo, na kwa dhahabu”.
Hapa tunaona jinsi Mungu anavyoweka ahadi ya kumbariki Abramu na kumfanya kuwa taifa kubwa. Kwenye sura ya 13 tunaona tayari Mungu ameshaanza kumbariki inasema alikuwa tajiri kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu. Bado katika 3Yohana 1:2 Mungu anasema “mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo .
Mpaka hapa tunaona kabisa ni mpango wa Mungu kutufanikisha katika mambo yote, hii ni pamoja na mafanikio ya kifedha. Na utajiri ambao Mungu anataka tuwe nao sio utajiri mdogo .
Sasa swali ni kwamba kwa nini Mungu anataka tuwe matajiri? Maana kuwa tajiri bila kujua sababu za kuwa na huo utajiri utashindwa kujizuia kwenye matumizi mabovu ya huo utajiri (Fedha). Huenda zipo sababu nyingi, lakini mimi nataka nikuonyeshe sababu tatu za kibibilia.
Sababu ya kwanza , kulinda mawazo na mikakati ya Mungu kwa watu wake.
 Yeremia 29:11. Mhubiri 7:12 “Kwa maana hekima ni ulinzi kama vile fedha ilivyo ulinzi na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliyo nayo” Mithali 18:11 “ Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake .
Kwenye kitabu cha Yeremia 29:11 Mungu anasema nayajua mawazo ninayowawazia, si mawazo mabaya, ni mawazo ya amani ………..Sasa ukiunganisha mawazo ya mhubiri 7:12 na mithali 18:11 utupata sentensi hii. Mungu anapokupa utajiri (fedha), anakutajirisha ili kulinda mawazo (mipango) na mikakati ya Mungu ambayo anakupa kabla ya kukupa hizo pesa kwa watu wake. Fedha yoyote ambayo Mungu anaileta mikononi kwako kumbe ina makusudi, mipango ya Mungu ndani yake.
Mungu anayo mipango na njia za kuwafanikisha watu wake kiuchumi, kimwili, kibiashara, kimaisha  n.k. sasa hii mipango inalindwa na nguvu ya fedha. Maana kama watu wake watakuwa masikini basi mipango aliyo nayo juu ya kanisa, familia, nchi n.k. basi si tu haitatekelezeka vizuri bali pia itanunuliwa na shetani kwa fedha yake. Hii ina maana Mungu anataka tuwe na nguvu ya kimaamuzi na ya utawala kwa yale anayotuagiza Mungu kwa sababu kwa fedha.
Sababu ya pili , Ili kuliimarisha agano lake.
kumbukumbu 8:18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, ili ALIFANYE imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Hapa tunaona wazi kabisa kwamba Mungu anasema ninakupa huo utajiri ili kulifanya agano lake kuwa Imara. Je agano hili ni lipi? Yeremia 31:31 inasema “Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, …. Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaindika; nami nitakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu wangu.
Agano ambalo Mungu anataka uimarishe kwa fedha anayokupa ni la yeye kukaa na watu wake. Maana yake tumia fedha anayokupa kujenga na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Yesu na watu wake.Uhusiano wa Yesu kama mwokozi, Rafiki, mpanyaji, Bwana n.k kwa watu wake maana yake ni hii, tumia fedha kufanya jambo lolote maadamu una hakika litapelekea uhusiano wa mtu (watu) na Yesu kuimarika na jina la Yesu kutukuzwa. Na kwa sababu hiyo utukufu wa mwisho wa nyumba hii/agano hili utakuwa ni mkuu kuliko ule wa kwanza, Hagai 2:8
Sababu ya tatu, ili tukopeshe na sio kukopa .
Kumbukumbu la Torati 28:12 inasema Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri … Nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe .Sikiliza tumeshaona katika mithali 18:11 kwamba mali ya mtu tajiri ni mji wake wenye nguvu… kwa lugha nyepesi maana yake fedha ya mtu tajiri ni nguvu ya huyo mtu kwenye mji aliopo/ au ambao yupo. Kwa kuwa akopaye ni mtumwa wake akopeshaye, hivyo utakapokopesha maana yeke utakuwa na nguvu juu ya maamuzi na hisia za huyo au hao watu uliowakopesha.
kama tukibakia kukopa tutakuwa watumwa na kwa sababu hiyo ndiyo maana Mungu anatupa utajiri kwa mtu mmoja, familia, kanisa, nchi n.k
Naamini sehemu ya kwanza ya somo hili litakusaidia katika matumizi ya utajiri ambao Bwana Mungu amekupa.
Ubarikiwe