Labels

Sunday, May 18, 2014

Tuwe makini, ndoa si jambo la mchezo!!


Katika maisha ya mwanadamu, kuna mambo mawili yaliyo muhimu zaidi. La kwanza ni uamuzi wa kumfuataYesu na la pili ni uamuzi wa kuoa. Tafakari, kuoa si sawa na kununua shati. Ukilichoka na shati unaweza kununua nyingine lakini, huwezi kumwacha mke wako hata kama ukimchoka. Neno la Mungu linatuonya hatari ya kuoa mwanamke asiye mchaji wa Mungu; Twasoma: “Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi” (Mithali. 21:19). “Kutonatona daima siku ya mvua nyingi, na mwanamke mgomvi ni sawasawa; 16atakaye kumzuia huyo huuzuia upepo” (Mithali. 27:15-16). Zingatia: Pengine mtu atasema, “mchumba wangu ana imani tofauti, walakini tukioana nitamfundisha.”Lakini ikumbukwe mara nyingi, baada ya kufunga ndoa, watu hubadilika asitake kufundishwa tena.Tukumbuke mfalme Sulemani alikuwa na hekima kuliko wanadamu wote. Walakini, alipata hasara kubwa kwa sababu aliwapenda wanawake wageni wasio mcha Mungu na matokeo yake badala ya kuwafundisha imani yake, “yeye mwenyewe alinaswa na imani yao” (1Wafalme 11:1-4). Basi tujiulize, je sisi tunayo hekima kuliko Sulemani? Ni bora mtu amfundishe mchumba kabla hawajaoana na kuhakikisha kuwa ameamua kumfuata Bwana kwa moyo wake wote na si kwa sababu ya ndoa, ndipo atakapokuwa na amani na furaha katika ndoa yake. Tukumbuke faida moja wapo ya kuoa katika katisa ni kupata mke alifundishwa maadili na wanawake waliomtangulia; Twasoma: “Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wautakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie – wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na uwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi,kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe, ili neno la Mungu lisitukanwe” (Tit. 2:3-5). Hivyo ni dhahiri kuna faida kwa mkristo kujipatia mke aliyefunzwa maadili ya ndani ya kanisa. Zingatia: Kuna baadhi ya watu wamevutwa sana na maumbile au mambo ya kimwili ya wachumba wao lakini Biblia inatukumbusha kuchunguza mioyo yao zaidi kuliko sura ya nje; Tasoma: “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa” (Mithali. 31:30). “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana” (Mithali 19:14). Je unazijua sifa za mke mwema? Mungu ameeleza peupe; Soma: (Mithali 31:10-31)
HATARI YA KUOANA NA ASIYE MCHAJI WA MUNGU
Kama tulivyojifunza hako juu hatari moja wapo ya kuoana na wasio wachaji wa Mungu ni kuishia kuvutwa na upotofu na kuanguka kiimani; Twasoma:”Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi” (Kumbukumbu 7:4). Na hayo ndiyo yaliyomapata Suleima kama tulikwisha kuoona; Soma tena: (1 Wafalme 11:1-4) Tukumbuke ikiwa tutaanguka katika uovu, mwisho wake utakuwa ni kutupwa katika hukumu (adhabu ya milele); Twasoma: “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uachafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui,ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayo fanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.” (Galatia 5:19-21) “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauwaji, na wazizi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili” (Ufunuo 21:8) “Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.” (Ufunuo 20:14- 15) Zingatia: Ndoa ni kifungo hivyo tukumbuke tunapoana hatuna ruhusa ya kuacha hata kama wenzi wetu ni wabaya vipi; Twasoma: “Lakini wale waliokwisha kuoana nawagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.” (1 Wakorintho 7:10-11) “Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumwe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu.” (1 Wakorintho 7:39)
Hivyo ni dhahiri tunaaswa kuwa makini tunapo wachagua wenzi wetu, tukikumbuka ya kuwa kifungo cha
ndoa ni mpaka kifo

No comments: