po umuhimu wa kujua neno la Mungu katika maisha ya Mkristo halisi.
Biblia inatuambia Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu. Kwa maneno mengine Yesu ndiye Neno ambalo Mkristo anapaswa kuwa nalo (Yohana 1:1).
Kwa kusema hivyo kuna umuhimu wa kumjua Yesu na kumshika, kwa maana yeye ndiye Neno la Mungu. Katika Biblia mtume Petro anasema mbele za Yesu kwamba, twende kwa nani na wewe ndio mwenye maneno ya uzima? Petro alijua upo umuhimu wa kumjua Yesu
| ||
Biblia inasema neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu (Wakolosai 3:16). Kwa nini basi neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu? Ni kwa sababu lina mambo yafuatayo ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya Ukristo. Mambo hayo ni… A) Neno la Mungu li Hai B) Neno la Mungu lina nguvu (Mwanzo 1:6). C) Neno la Mungu lina ukali kuliko upanga D) Neno la Mungu linachoma hata kuzigawanya nafsi, roho viungo na mafuta yaliyomo ndani yake E) Neno la Mungu li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo Neno la Mungu li hai kwa sababu Mungu mwenyewe analithibitisha kwamba li hai maana a) Linafanya mabadiliko (Isaya 55:10-11). b) Linatupa kushinda dhambi (Zaburi 119:11). c) Neno la Mungu li hai kwa sababu linatupa mafanikio katik mwili. Petro anasema ”kwa neno lako tunatupa nyavu zetu.“ Hapa tunaona kuwa Neno la Mungu pekee yake ndilo linaloweza kuleta majibu katika maisha yetu (Luka 5:3-6). Yesu kama kielelezo yeye mwenyewe ni neno ndani ya neno anamshinda shetani (Luka 4:1-12). Yesu kama Neno la Mungu anajua mambo ambayo watu wanawaza ndani ya mioyo Wokovu wetu unaimarika kwenye neno la Mungu. **************** au nipigie simu: 0764618028; Mungu akubariki |
BIBLIA NI NENO LA MUNGU LILILO HAI
Katika Biblia Yako SomaZaburi 119: 9-11,105;
Waebrania 4:12; Marko 4:21-29.
Mstari Wa KukaririKila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema (2Tim 3:16, 17).
Baadaye Zungumzieni Jambo HiliJe, unaamini kuwa Neno la Mungu ndilo lenye mamlaka yote katika maisha?
Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana TenaJitahidi kutenga muda maalum kila siku kwa ajili ya kutulia na kutafakari. Tekeleza mpango wa kusoma Biblia. Andaa alama saba za kuweka katika Biblia yako pale unapoachia kusoma ili uweze kupapata kirahisi utakapoendelea kupasoma tena wiki inayofuata.
Kazi Ya Kuandika Ya StashahadaKutoka katika 2Fal 22:8-13 na 2Fal 23:1-32 andika mageuzi yote aliyoyafanya mfalme Yosia baada ya kulisikia neno la Mungu.
Tafakari Andiko HiliMathayo 7:24-27
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Ujerumani.
Idadi ya watu: 80,000,000. Idadi ya Wakristo ni 75%
Ujerumani Mashariki maskini na Ujerumani Magharibi tajiri sasa zimeungana. Makanisa ya zamani yanapoteza watu. Uamsho unatakiwa haraka
Kwa kila mwamini neno la Mungu ni la kipekee na la thamani kubwa. Kwa karne nyingi zilizopita watu wengi wametoa maisha yao katika kuhifadhi kweli ya neno la Mungu kwa ajili yetu ili tupate kusoma. Kwa kuzingatia thamani kubwa ya neno la Mungu, na andiko kutoka Mk 4:21, swali ni hili, ‘Biblia iko wapi katika maisha yako?’
Je, imefichwa mbali;
Au imewekwa mahali pa juu ili ipate kumulika kila eneo la maisha yako?
2. Baraka Katika Neno La MunguNeno lake li hai, linanena nawe na kutenda kazi ndani yako (Ebr 4:12,13).
Neno lake ni kioo kinachokufanya ujione ulivyo kadiri unavyoendelea kulisoma. Neno lake kamwe halitakufanya ujidanganye mwenyewe, wala kuficha ukweli (Yak 1:22-24) (Mk 4:22).
Neno lake litakuandaa kikamilifu ili uwe, na ufanye kile Mungu anachotaka (2 Tim 3:15-17).
Kuanzia ulipokuwa mtoto hadi sasa umeyajua Maandiko Matakatifu yanayoweza kukupa hekima unayoihitaji kwa ajili ya kupata wokovu kwa imani katika Kristo Yesu. Maandiko yote yana pumzi ya Mungu nayanafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Inasemekana, na ndivyo ilivyo, kwamba Biblia ni Mwana wa Mungu katika maandishi, kwa sababu Yesu anaitwa ni Neno, na vilevile anaitwa Kweli (Yn 1:1).
Je, Unataka Kufanikiwa Na Kustawi?Basi fanya yale Yoshua aliyoagizwa kufanya (Yos 1:8). Na kama unataka kustawi kwa kila kitu zingatia Zab 1:1-3.
3. Je, Unaposoma Unasikia?
Je, umewahi kugundua kuwa unaposoma neno la Mungu ‘unasikia’ kwa ndani na si kwa masikio ya nje? Hiyo ni sauti ya Mungu. Yapasa tuwe makini na kile tunachosikia kwa sababu kwa kipimo kilekile tunachotumia, ndicho tutakachopimiwa (Mk 4:24).
4. Je, Unalitumiaje Neno La Mungu?
Unalitumia hilo neno kufanya upya moyo wako (Rum 10:17).
Unalitumia hilo neno kufanya upya mawazo yako Rum 12:2).
Unalitumia hilo neno kufanya upya maneno yako (Rum 10:10) (Mit 18:2).
Ulitumie hilo neno kufanya upya matendo yako (Yn 14:15).
Ulitumie hilo neno kuimarisha ushindi wako. Shetani hakuwa na usemi Yesu aliposema, ‘Imeandikwa’! (Mt 4:1-11)-zingatia mistari ya 4,7 na 10.
Litumie Neno Kuhuisha Maombi YakoWaamini wa kwanza mara kwa mara walinukuu maandiko ili yawaongoze katika maombi, na Mungu alijibu haraka (Mdo 4:23-31). Iwapo utaomba kwa kutumia neno la Mungu, yafuatayo yataanza kutokea:
Kwanza, unapanda mbegu ya neno.
Kisha kwa uvumilivu katika kuliomba neno, na saburi, huja masuke. Na kwa kadiri unavyoendelea kuwa na imani kwa Mungu na katika neno lake, huja ngano pevu, nafaka kukomaa na hatimaye mavuno.
(Mk 4:14, 26-29) (Isa 55:10, 11) (Mwa 8:22).
Ni Muhimu Kuwapa Wengine Neno La MunguNi muhimu kwa sababu ye yote mwenye neno la Mungu anaweza kuokolewa na kupewa zaidi, mathalani: uponyaji, uhuru, uongozi, baraka na ustawi, kwa kuliamini. Lakini mtu asiye na hilo neno la Mungu ili kuliamini na kulifanyia kazi, hana baraka yo yote katika hizo zilizotajwa, na atapoteza hata hicho alichonacho, yaani maisha yake na nafsi yake milele (Mk 4:25).
5. Unapataje Kulisikia Neno?Mungu amefanya iwe rahisi sana kuisikia sauti yake. Wewe kaa peke yako na Yeye, na kisha fungua Biblia yako. Kiri udhaifu wako na omba kujifunza kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Chukua muda kutafakari yale uliyosoma na kusikia, kwa sababu kwa njia hiyo utashangaa kuona jinsi Mungu atakavyozungumza na wewe na kujibu maswali yako.
Nikiwa mwamini mpya sikuyajua mambo haya. Nilihudhuria kwenye kusanyiko la maombi na kimyakimya niliomba kwa ajili ya kazi yangu, nikamwombea mke wangu na watoto kwa sababu ya matatizo yote tuliyokuwa nayo. Baada ya muda mfupi nilihisi msukumo wa kuichukua Biblia yangu na ikafunguka yenyewe katika Zaburi ya 128. Na nilipoanza kusoma Mungu alinistusha na baadaye akanipooza kwa neno lake akiuambia moyo wangu:
“Wamebarikiwa wote wamchao Bwana na kutembea katika njia zake.
Utakula matunda ya kazi yako, baraka na kustawi vitakuwa vyako.
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, na wanao kama matawi ya mtende mezani pako”.
Naliliamini neno la Mungu na leo hii, baada ya miaka kadhaa kupita naweza kuona jinsi Mungu alivyoitunza ahadi yake kwa kuibariki familia yangu na kazi yangu.6. Namna Ya Kufurahia Usomaji Wa Biblia
Watu wengi huanza na kitabu cha Mwanzo na baadaye huacha wanapokutana na sehemu ngumu katika Agano la Kale ambazo hawazielewi. Sisi sote tunapenda kula vyakula mbalimbali siku kwa siku, na hivyo ndivyo ilivyo hata kwa chakula cha kiroho. Jaribu kufuata mpangilio ufuatao nawe utapata mlo tofauti kila siku. Kila siku soma Zaburi za kuabudu na Mithali kwa ajili ya kupata hekima.
Jumatatu
Hadithi za watu mashuhuri na za historia ya Biblia. Anza na kitabu cha Mwanzo na kuendelea hadi kitabu cha Esta.
Jumanne
Taarifa za watu waliomjua Yesu vizuri. Anza na injili ya Mathayo na kuendelea hadi ya Luka.
Jumatano
Tembea katika vilima na mabonde ya ushairi. Anza na kitabu cha Ayubu hadi Wimbo Ulio Bora.
Alhamisi
Nyaraka za upendo kutoka kwa Yohana. Anza na injili yake, ikifuatiwa na nyaraka zake, na kuishia na Ufunuo wake.
Ijumaa
Unabii wa Biblia. Anza na Isaya na kuendelea hadi Malaki; utastaajabu.
Jumamosi
Nyaraka kutoka kwa watu mashuhuri wa Mungu. Anza na Warumi, endelea hadi Petro na Yuda.
Jumapili
Tembelea makanisa yaliyo hai na misheni zilizoko mstari wa mbele kwa kusoma kitabu cha Matendo ya Mitume.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina
UWEZA WA JINA LA YESU
Mtume Paulo anasema katika Waraka wake kwa Wakolosai sura ya tatu na mstari wa kumi na saba kuwa; “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika JINA LA BWANA YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.”
Hii ina maana ya kuwa, tukila tule katika Jina la Yesu Kristo. Tukilala tulale katika Jina la Yesu Kristo. Tukizungumza tuzungumze katika jina la Yesu Kristo. Tukiimba tuimbe katika jina la Yesu Kristo. Tukitembea tutembee katika jina la Yesu Kristo. Tukisafiri tusafiri katika jina la Yesu Kristo. Tukilima shambani tulime katika jina la Yesu Kristo; na kadhalika.
Kwa nini tunatakiwa tufanye mambo yote katika jina la Yesu Kristo? Jina hili la Yesu Kristo lina sehemu gani katika maisha yetu ya kila siku?
Kama tunatakiwa kufanya mambo yote katika jina la Yesu Kristo, kwa nini hatufanyi hivyo?
Ukitafakari maagizo tuliyopewa katika biblia utaona ya kuwa, maisha yetu yote yanalitegemea jina hili la Yesu Kristo.
Kama mambo yetu yote yanatakiwa yafanyike kwa jina la Yesu, basi ni muhimu tujifunze zaidi na zaidi kila siku juu ya jina hili la ajabu.
Ni maombi yangu kwa Mungu Baba, katika jina la Yesu Kristo ya kuwa maneno yaliyomo katika somo hili yatachochea kwa upya kiu iliyomo ndani yako ya kutaka kufahamu zaidi siri iliyomo ndani ya jina la Yesu Kristo.