Mt. Meshack Ezekia Kitova phone;0757672626
Nini maana ya kusifu na kuabudu
KUSIFU NA
KUABUDU ni maneno tofauti na yana maana tofauti
1.
kusifuMAANA --- nikuelezea wasifu au wajihi za kitu au mtu.
Sasa tunaposema tunamsifu Mungu inamaanisha ni KWA KUMUINUA JUU, KUSHUKURU
KUMPAZIA SAUTI,KUFANYIA SWANGWE, KUJISHUSHA CHINI YAKE KWA UNYEYEKEVU,nk Zaburi
100:4
Neno hili kusifu kwa kiebrania lilikuwa na maana ya;
Tehila,
yaani kutamka neno kwa kuongeza vionjo na mbwembwe zaidi. Mfano neno haleluya
unalitamka (Ha, ha leluya huuu eee) Tehila ni kuwa kama kichaa unaposifu au
kuabudu kwa utukufu wa Bwana. (Nilidhani labda hapa ndipo waswahili walipopata
neno taahila).
Yadaa yaani kujiachia kwa Mungu (you just surrender
yourself to the Lord).
Barak yaani kusaluti mbele za Bwana. Ni kuonyesha
kwamba ni yeye peke yake anayestahili heshima na utukufu. Huwezi kumpigia saluti
mtu usiyemwona, hivyo ni kwa njia ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli ndipo
tunapomwona kama alivyo na utukufu wake
2. Kuabudu
Neno la Kiebrania shachah lina maana ya kuabudu, kusujudia, kuinama
kwa kuonesha unyenyekevu, kuonesha heshima kubwa au kuanguka kifudifudi. Neno la
Agano la Kale proskuneo halikadhalika lina maana ya kubusu mkono, au kupiga
magoti na kugusa ardhi kwa paji la uso kwa unyenyekevu mkuu. Maneno mengine
mawili ya kuabudu yana maana ya kutumika, kufanya ibada Takatifu na kumtolea
Mungu Sadaka.
Waache Watu Wangu Waondoke, Ili Wapate Kunitumikia, Dai
hili Mungu alilolirudia mara kwa mara lilipelekea Farao kuwaruhusu watu wa Mungu
kutoka Misri. Tangu wakati huo, Mungu, Mungu mwenye wivu, amekuwa akipambana na
watu wake akiwazuilia kuabudu miungu mingine na sanamu, na badala yake wamwabudu
Mungu aliye hai na wa kweli. Kutoka 7:16
Ibada ni kumtukuza Mungu na
kumfurahia daima. Mungu anawatafuta watu wa kumwabudu, na kufanya ibada ndiyo
wito wetu wa kwanza (Yn4:23 Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo
halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio
Baba anawatafuta. Msitari wa 24 unasema Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu
imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.). Ibada ya kweli ni pale tunapomruhusu
Roho Mtakatifu atuongoze kutoka katika roho zetu au mioyo yetu kuabudu katika
roho na katika kweli na sio tumaini letu ktk miiliau akili zetu Flp
3:3.
Ibada ni tendo la thamani kubwa, ni la kipekee na linamhusu Mungu
(utatu mtakatifu) ambao peke yao wanastahili. Lucifer, aliyekuwa mhusika mkuu wa
ibada huko mbinguni, alitaka ibada hiyo iwe kwa ajili yake, maana yake aabudiwe
yeye badala ya Mungu; na hilo ndilo lililopelekea kuanguka kwake (Isaya 14 na
Ezekieli 28). Hata wakati fulani alitaka Yesu amsujudie ili eti ampe falme zote
za dunia lakini Bwana alikataa Mt4:8-10.
Kwa hiyo kuabudu ni ibada na
tunaposema ibada sio zile taratibu za kibinadamu tulizojipangia katika ibada
zetu za siku za leo, ibada za leo tumeweka mambo mengi sana na yanatumia muda
mwingi sana kuliko ile maana hasa ambayo mungu aliikusudia katika agano la kale
utana ibada zilikuwa zinafaywa kwa mambo makuu 2 neno la Mungu, na
Kuabudu.
Kuabudu ni sehemu ya maisha wanadamu tumeumbiwa kuabudu,
watuwezi kuishi bila kuabudu hapa haijalishi unaabudu nini!!! Unaweza kuwa
unaabudu Mungu wa kweli au miungu kama ambavyo ukisoma bilia utaona kuna miungu
mingi inatajwa mfano Baali, Dagon ink na hata leo iko miungu mingi ambayo
wanadamu wanaiabudu lakini wa kuabudiwa ni mmoja tu. Na katika biblia tunaona
kuaudu kwa mara ya kwanza kulikofanywa na Ibrahimu kutoka katika kitabu cha
mwanzo 12: 8 Psalms 34:1 inaonyesha tunatakiwa kumwabudu Mungu kila
wakati.
Kwanini tuabudukuabudu ni agizo kutoka kwa
Mungu kutoka 20 2-4 . Psalm 96:9, Psalm 29:2 Tunapomwabudu mungu naye Mungu
hufurahiwa na sisi Zephaniah 3:17 Rom 12:1-2
Your Worship = Your
View of Godjinsi unavyoabudu ndiyo mwonekano wa mungu ulivyo ndani
yako, haijarishi unaabudu wapi uwe peke yako au mko wengi kama unaabudu kwa
kutokumaanisha au kumaanisha itajulikana tu na hivyo ndivyo mtu anaweza kujua ni
jinsi gani mtazamo wako kwa Mungu wako.
KUNA NGUVU KATIKA KUSIFU
NA KUABUDUYoshua 6:20 Matendo 16:23-26 zinaonyesha ambavyo kwa
kutumia kusifu tu Mungu alishuka na kufanya lile lililokuwa hitaji
lao.
Kusifu kunamfukuza aduiPsalms 50:23. 2 Nyak
20:22. Ukiwa unasifu na kuabudu humfukuza adui mbali kutokana na ukiwa kwenye
ibada Mungu hushuka maana yeye anasema anakaa katikati ya sifa hivyo palipo na
Mungu shetani hawezi kuwepo lazima akae mbali.akimbie mbali kabisa maana
kunakuwepo na uwepo wa bwana wa Majeshi.
Je, ni wakati gani
tuabudu?Ni niyakati zote zinafaa kumwabudu Mungu. Kwa nyakati
zilizotengwa Zaburi ya 100 inatuelekeza namna ya kuanza, lakini zaidi ya yote
tunapaswa kuishi maisha ya ibada bila kukoma. Kwa kila tunapopumua, kwa kila
wazo, kwa neno na tendo, tunapaswa kumwabudu Mungu wetu mzuri tunayemtumikia
milele na milele Zab 145:1,2
mwa 12:6- Siku zilipita na watu wakafanyia
ibada kwenye Hekalu na kwenye masinagogi; lakini siku hizi miili yetu ni hekalu
la Mungu 1Kor 6:19 tu hekalu la Mungu sisi ibada zinatakiwa zifanyike kila
wakati na si mara moja kwa wiki kama wengine wanavyo dhani.
Je,
Tunafanyaje Ibada?Biblia inatufahamisha jinsi watu walivyotumia
mioyo yao, mawazo yao, mikono yao, viganja vyao, miguu yao, na midomo yao katika
uimbaji. Walipaza sauti zao kwa furaha na kusujudu, kucheza, kusifu, kubariki na
kushukuru.
Maneno kama halal na haleluya kutoka katika Zaburi yana maana
ya kusifu, kumwinua na kumwadhimisha Bwana. Neno Yadah lina maana ya kunyoosha
mikono hewani, na neno barak lina maana ya kupiga magoti katika ibada ya
kumbariki Mungu. Kuitoa miili yetu katika kumhudumia Mungu na mwanadamu ni ibada
pia (Rum 12:1). Watu pia humwabudu Mungu katika sanaa zao, katika uandishi wao,
katika michezo ya kuigiza, katika muziki, katika usanifu wa majengo, na hata
katika utoaji wa fedha zao kwa ajili ya Injili.
Kusifu na kuabudu
sio kuimba tuWatu wengi wanajua kuwa kusifu na kuabudu ni kuimba tu
hapana kuna njia nyingi za kusifu au kuabudu, unaweza kutumia sanaa nyingine
kumwabudu mungu au watu wengine wakamwabudu Mungu mf maigizo, ngonjera, shaili,
uchoraji, upambaji au unakshi wa vitu, kujenga .nk
Ibada
KanisaniKatIka kanisa makusanyiko yetu yanapaswa kujawa na zaburi,
nyimbo, na tenzi za rohoni ambazo zinaweza kuongozwa na Roho katika lugha mpya
anazotupatia Yeye. Kwahiyo mikutano mingi ya kisasa haina tofauti sana na
burudani za kikristo kama kwenye kumbi za starehe. Watu huwa wanaangalia tu,
lakini je, wanaabudu? Uwepo wa Mungu na Roho wake katika ibada zetu utawafanya
watu wasioamini kuanguka chini na kuabudu (Kol 3:16) (1Kor 14:15,16,25,26) (Efe
5:19) (Mdo 2:4).
Ibada Ya Kweli Ina GharamaBiblia
inazungumzia habari za sadaka za kusifu. Daudi alicheza mbele za Bwana kwa nguvu
zake zote, na akakataa kumtolea Mungu kafara ambayo isingemgharimu cho chote
(2Sam 6:14; 24:24). Wale mamajusi wa Mashariki walitoa zawadi za gharama kubwa
walipokuja kumwabudu Yesu (Mt 2:9-12), na mwanamke mmoja alimpaka Yesu kwa
mafuta ya gharama kubwa, akamwosha miguu yake kwa machozi yake, na kuifuta kwa
nywele zake (Lk 7:36-50). Hivyo ibada yoyote inaambatana na kutoa tena vitu
vyetu vya thamani.
Tunapaswa kumsifu Mungu kwa jinsi alivyo na kwa
matendo yake; lakini Mungu mwenyewe anawatafuta na anawataka wafanya ibada, na
si mradi ibada tu. Kusifu kwaweza kufanywa hadharani, lakini ibada mara zote ni
jambo la ndani ya moyo. Kusifu mara zote kunaweza kuonekana au kusikika, lakini
kuabudu yaweza kuwa ya kimyakimya na iliyofichika. Kusifu kunaonekana, kuna
kutumia nguvu, kuna misisimko na furaha; lakini ibada mara zote ni heshima na
hofu katika uwepo wa Mungu.
Biblia pekee inatuonesha jinsi Mungu anavyo
hitaji na kutamani kuabudiwa na yeye pekee yake ndiyo anayestahili
kuabudiwa.
Kusifu na kuabudu kwa siku za leoKatika
siku za leo kuna ufinyu wa mafundisho katika kusifu na kuabudu na ndiyo maana ya
kuanda somo hili ili tupanuane mawazo. Watu wengi wa leo wanadhani kusifu ni
kuimba kwa nyimbo zenye midundo ya harakaharaka(zouk&sebene) na ukipunguza
spidi ndo kuabudu. Hasha tunaposema kusifu inatokana na maneno yaliyopon kwenye
wimbo husika kweli ni ya kusifu, kama ni maneno ya kusifu tunasema ni wimbo wa
sifa haijarishi speed inayotumika na hali kadhalika nyimbo za kuabudu. Watu
katika kipengele hiki huwa wanachakanya nyimbo utakuta wakati wa kusifu anaimba
wimbo wa kutia moyo au wa maombi, kinachotakiwa ni kujua kuwa kila jambo lina
wakati wake ziiko nyimbo za mazishi, kufariji, kutia moyo, za maombi, za kusifu
, na za kuabudu nk sasa usichanganye kwenye kusifu wewe unaimba parapanda italia
au tuonane paradiso, hizo sio za sifa sasa najua wewe utafanya zoezi la nyimbo
unazozijua ili kufahamu zina ujumbe gani na ziko katika kundi lipi kati ya hayo
niliyokufundisha hapo juu.
Baadhi ya maandiko yanayo onyesha
aina za kusifu na kuabudu kwa: 1. Kusimama (Zab 135:1-2, 134:1)
2. Kuinua mikono (Zab 134:2, 28:2)
3. Kuinama au kupiga magoti
(Zab 95:6)
4. Kupiga makofi (Zab 7:1)
5. Kucheza (Zab 149:3,
150:4, 2Sam 6:14)
6. Kicheko (Zab 126:2, Ayu 8:20-21)
7. Kufurahi
(Kumb 12:11-12, Law 23:40)
8. Kutembea (2Nya 20:21-22)
9. Shangwe
(Zab 95:1)
10. Kupiga kelele (Zab 66:1, Law 9:23-24)
11. Kupiga
vigelegele (Zab 33:1, 32:11)
12. Ukimya (Mhu 3:7)
13. Kupaza
sauti (Isaya 12: 6, Zab 42:4)
14. Kulia/ kutoa machozi katika roho
mtakatifu
Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo
mengine mtazidishiwa